Kikosi cha Simba
chini ya kocha wake, Joseph Omog kimeendelea na mazoezi mjini Morogoro
kujiandaa na mechi yao ya keshokutwa ya Kombe la Shirikisho jijini Dar
es Salaam.
Simba itakuwa mwenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mechi inayotarajiwa kuwa ngumu.
Mratibu wa Simba,
Abbas Ally ‘Gazza’, amesema wanaendelea na maandalizi vizuri na uongozi
unatimiza majukumu yake kuhakikisha vijana wanafanya vizuri.
“Kila kitu kinakwenda
vizuri, kila kitu kipo kamili na hakika vijana wanajituma kweli. Lengo
ni kufanya vizuri katika mechi hiyo,” alisema.
“Kila mmoja wetu anajua ni mechi ngumu na muhimu, hivyo kikubwa ni kuendelea kujituma kwa juhudi zaidi.”
No comments:
Post a Comment