Kwa takribani miaka miwili mfululizo, nywele aina ya Rock Dread
zimeendelea kushika kasi zaidi na kupendezesha muonekano wa mtu yoyote.
Mtindo huu wa nywele umekuwa ukifanya vizuri tangu ulipoanza
kuoneakana vichwani mwa watu, na kwa hapa nyumbani, mtindo huu wa nywele
umetumiwa na watu mbali mbali wakiwemo watu maarufu hata wasio maarufu.
Kifaa maalum hutumika katika kuzisokota nywele hizo na pia mafuta aina ya gel hutumika kutengeneza nywele za Rock Dread.
Rock Dread huhusisha zaidi nywele zilizo fupi za asilia, yaani
natural hair. Hii ni kwa sababu, hutulia vizuri kichwani na kudumu kwa
muda mrefu. Imekuwa ni kawaida kukuta kati ya kundi la watu kumi,
kutokukosa wawili wakiwa na Rock Dread.
Aina hii ya nywele pia hutumika kwa watu wa jinsia zote. Wataalamu wa
maswala ya mitindo wanaamini kuwa, stlye hii ya nywele ina uwezo wa
kukaa muda mrefu zaidi katika akili na machoni mwa watu.
Zifuatazo ni njia fupi na rahisi za kutengeneza aina hiyo ya nywele:
a) Hakikisha umekata nywele zako.(Hapo unaweza pakaa rangi ya nywele endapo utapendelea).
b) Pakaa mafuta maalum ya kutengenezea mtindo huo wa nywele kwenye nywele zako.
c)Tumia kifaa cha kutengenezea ynywele hizo kijulikanacho kama Twist
No comments:
Post a Comment