• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 9 April 2017

    Malim sefu aibua mampya sakata la lipumba

    Katibu wa chama cha wananchi Cuf  Maliim sefu amekemea vitendo vinavyo endelea kwa upande wake baada ya kutokea mgogoro baina yake na mwenyekiti wake prof Ibrahim Lipumba.

    Maalim Seif leo Aprili 9,2017 jijini Dar es Salaam ameibuka na kueleza hujuma tano nzito alizodai zimetekelezwa na Lipumba kwa kushirikiana na vyombo vya dola, kwa kutumia mgongo wake kukidhoofisha chama hicho, huku akijinasibu kuwa hajashindwa kutekeleza majukumu yake na kuahidi kwamba mara baada ya kumaliza ziara ya ujenzi wa chama Zanzibar atahamia Bara ili kudhihirishia wanachama hajashindwa kufanya kazi.
    Hata hivyo, ametangaza vita dhidi ya Profesa Lipumba na kundi lake huku akisitiza kuwa yeye bado Katibu Mkuu hadi pale atakaposimamishwa na Baraza Kuu la Uongozi halali la chama hicho au kufukuzwa uanachama na Mkutano Mkuu halali wa CUF.
    “Tumevumilia vya kutosha sasa basi, tutailinda CUF kwa gharama yoyote ile na nyie mlio nyuma ya mgogoro huu mtabeba dhamana kwa mliyoyatenda. Hakuna tena cha kunitisha na kunikatisha tamaa na tulipo fika tutapata ushindi,” amesema.
    Miongoni mwa hujuma tano alizotaja Seif dhidi ya CUF, ni pamoja na vyombo vya dola kumzuia kufanya shughuli za kisiasa upande wa Tanzania Bara, Lipumba kuvamia na kuteka baadhi ya ofisi za CUF, wizi wa fedha za ruzuku, na Bunge kupokea wagombea feki wa chama hicho katika uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.
    Licha ya hayo, Maalim Seif ameitaka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kutokubali kushiriki njama ovu aliyodai kuwa imelenga kusajili wajumbe feki wa Bodi ya Wadhamini CUF kwa minajili ya kumlinda Lipumba na Kundi lake ikiwemo kufuta kesi zilizofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya chama hicho dhidi ya mwenyekiti huyo anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na wenzake ambazo zimelenga kukilinda chama hicho.
    Hali kadhalika amesema kuwa, CUF imekwisha pitia migogoro mingi ambayo chama hicho imeshinda kwa kuwa ni taasisi imara na kudai kwamba mgogoro uliopo sasa haujalenga kukisambaratisha chama hicho pekee bali umelenga kuiua demokrasia nchini kwa kukandamiza na kuzuia taasisi za kidemokrasia Tanzania kutekeleza majukumu yake.
    “Huu ni wakati wa wapenda demokrasia na wapenda amani wote kusimama pamoja 

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI