• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 8 April 2017

    Dc Ilala azuia kuchimba mawe katika machimbo ya golani


    Dc wa Ilala Sophia Mjema akishirikiana  na jeshi la uokoaji wamefanikisha kuokoa mwili wa Rashidi Fadhili na kuu wacha mwili wa bonfasi baada ya jitihada zote kufanyika katika machimbo ya mgolani kigogo fresh jijini dar es salaam

    Jitihada hizo zimefanyika takribani Siku mbili mfululizo baada ya kupata taarifa ya kufukiwa watu hao


    Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesitisha zoezi la uokoaji mtu mmoja aliyebaki kwenye machimbo ya kokoto Golani, yaliyopo Pugu Kigogo Fresh, mkuu wa wilaya huyo ameeleza kuwa wameamua kusitisha zoezi hilo kwakuwa eneo hilo ni hatari na udongo unaweza kuanguka zaidi na kuleta athari kwa watu wengine.

    DC Mjema amesisitiza kuwa baada ya kuyafunga machimbo hayo anawaomba wakazi wa eneo hilo kuhamisha viroba vyao vya kokoto, chepe  kwa muda wa siku mbili na asionekane mtu katika eneo hilo, huku akisisitiza kuwa serikali imejitahidi katika zoezi hilo la uokoaji kwani imeweza kuokoa watu watatu ambapo wawili waliokutwa wamefariki na mmoja alikuwa amejeruhiwa mguuni

    DC Mjema amesema zoezi hilo la uokoaji lililofanyika siku ya leo wamefanikiwa kuokoa mwili wa marehemu Fadhili Rashidi, huku mwili wa Boniphace Pius wakishindwa kuuokoa kutokana na eneo hilo kuwa na hatari zaidi baada ya udongo kuanza kuporomoka.

    DC Mjema ametoa pole kwa familia ya wote walioondokewa na ndugu zao baada ya tukio hilo la juzi kuwa na madhara makubwa kwa familia hizo, ambapo kwa upande wa familia hiyo Baba Mdogo wa Boniphace Pius ambaye mwili wake umebaki katika machimbo hayo Aloyce Mlawa amesema wameridhika na juhudi za serikali katika uokoaji na wameridhia kusitishwa kwa uokoaji huo na kuamua kufanya maombi kwa ajili ya ndugu yao huyo ambaye hajabahatika kuokolewa kutokana na hali ya hatari katika eneo hilo.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI