Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
ametahadharisha kuwa, wapo mbioni kuhakikisha mapato ya serikali
yanadhibitiwa zaidi ili taifa liweze kujitegemea kikamilifu, huku
akionya makampuni ya simu nchini.
Rais Magufuli ameyasema hayo Ijumaa hii, mjini Dodoma wakati
akikabidhiwa taarifa ya vyeti feki. Rais ameyaonya makampuni hayo,
akisema, dawa ya makampuni hayo bado inatengenezwa.
“Bado kuna maeneo mengi ambayo tunaibiwa fedha. Kwenye haya makampuni
ya simu haya, yanafanya transactions nyingi lakini hela haziingii
serikalini, dawa yao tunaitengeneza baada ya muda mfupi kidogo
itakamilika,” alisema Rais Magufuli huku akishangiliwa.
No comments:
Post a Comment