MABANDA 13 yanayouza mbao katika soko la Kambarage mjini Shinyanga
yameteketea kwa moto na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kwa
wafanyabiashara wa mbao.
Tukio hilo limetokea jana saa 5.30 usiku, ambapo moja ya banda ndio
lilianza kuungua na hatimaye yote yakashika kasi kuwaka na kuteketeza
mbao zote.
Mmoja wa walinzi wa mabanda hayo Faustine Mapuli, alisema wakati
akizungukia lindo lake gafla akaona moto ukiwaka kwenye banda moja na
hivyo kuwaita wenzake na kuaanza kuuzima kwa kuumwagia michanga, lakini
walipomwaga maji ndipo ukalipuka na kuwazidi.
Alisema baada ya kuwazidi walipiga simu kwa wamiliki wake ambao ndio
wakatoa taarifa Jeshi la Zimamoto ambao walifika eneo la tukio
kujitahidi kuuzima lakini wakati huo mbao zote na mashine za kulandia
zikiwa zimeshaungua kutokana na moto huo kuwa mkubwa.
Naye mmoja wa wamiliki wa mabanda hayo Mosesi Mizungu, alisema kutokana
na tukio hilo amepata hasara zaidi ya Sh. Milioni 15 jna kupoteza
nyaraka mbalimbali za biashara yake zikiwamo za mikopo na madeni ambayo
anadai wateja wake
No comments:
Post a Comment