Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako
amesema kwamba suala la uhakiki wa vyeti feki nchini tangu Tanzania
ipate uhuru ni mara ya kwanza zoezi la uhakiki kufanyika huku
akisema,ngoma bado mbichi.
Profesa Ndalichako, ameyasema hayo mjini Dodoma wakati wa kumkabidhi
Rais Magufuli taarifa ya majina ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.
“Mheshimiwa Rais, suala la uhakiki wa vyeti umefanyika kwa mara ya
kwanza, tangu nchi yetu ilipopata uhuru, tunakupongeza sana kwa
kuonyesha uongozi thabiti kwa vitendo. Kwakweli huna kigugumizi katika
kufanya maamuzi, na tunakupongeza sana. Mheshimiwa Rais, wizara yangu
imetekeleza maelekezo ya serikali kwa kuhakiki vyeti vya kidato cha nne,
cha sita na vyeti vya ualimu katika ngazi ya cheti na stashahada kwa
watumishi wa umma nchini,”alisema Ndalichako.
“Kwa hiyo naomba mnisikilize vizuri, tumehakiki vyeti vya kidato cha
nne na cha sita kwahiyo kwa maneno haya, ngoma bado mbichi maana yake
vyeti vya taaluma bado hatuja hakiki. Matokeo tunayoyawakilisha leo
(jana) ni ya uhakiki wa vyeti kidato cha nne, cha sita na vyeti vya
ualimu kwa watumishi wa umma.”
Aidha Ndalichako aliwaasa wanafunzi wote nchini kusoma kwa bidii, na kuongeza njia zote zimefungwa.
No comments:
Post a Comment