• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 4 April 2017

    RCMAKONDA ; TAKUKURU imepewa wiki mbili kuchunguza na kuwafikisha Mahakamani watu wote waliokiuka utaratibu na kufanya ubadhilifu wa zaidi ya shilingi Bilioni-7

    Image result for makondaTaasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa-TAKUKURU imepewa wiki mbili kuchunguza na kuwafikisha Mahakamani watu wote kuanzia Mtendaji wa Mtaa mpaka kwenye Ofisi ya Mthamini wa Serikali Mkuu waliokiuka utaratibu na  kufanya ubadhilifu wa zaidi ya shilingi Bilioni-7, fedha ambazo zingetumika kulipa watu wasiostahili kupitia mradi wa Maendeleo ya jiji la Dar es Salaam maarufu kama DMDP.


    Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam PAUL MAKONDA, ametoa agizo hilo wakati akizungumzia na wandishi wa habari kuhusu miradi inayototekelezwa Mkoani humo ikiwemo ya DMDP, huku akisema tayari ameshaiandikia barua TAKUKURU ili kutekeleza agizo hilo.
     MAKONDA alisema, kuwa Wilaya Ilala na Temeke ndizo zimeongoza kwa kukiuka taratibu na kufanya ubadhilifu wa zaidi ya shilingi Bilioni-5 na Kinondoni zaidi ya shilingi Bilioni-1.
     Kwa upande wa Temeke na Ilala hali hiyo imebainika baada ya kutaka kujiridhisha na kuweka kumbukumbu sawa kabla ya kusaini vitabu kwa ajili ya kupitisha fedha za miradi ya DMDP ambapo baada ya kufanya uchunguzi ikagundulika kwamba vitabu Vinane vimekiuka taratibu na masharti.
             
    Miradi ya DMDP inahusika na ujenzi wa Barabara, Miferreji na uboreshaji wa jiji la Dar es Salaam.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI