• Breaking News

    ..

    ..

    Tuesday, 4 April 2017

    WAZIRI MKUU MAJALIWA MGENI RASMI MAONESHO YA MIFUKO YA UWEZESHAJI WANANCHI.

    NEE1
    Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akizungumz ana waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya Maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.
    NEE2
    Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akimskiliza Mhasibu Mkuu kutoka Mfuko wa Rais wa kujitegemea Bw.Ahazi Kibona juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.
    NEE3
    Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi.Beng’I Issa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji kutoka Mfuko wa Pembejeo na Zana za kilimo wa Taifa Bi.Mariam Nkumbi juu ya shughuli mbalimbali zitokanazo namfuko huo.
    Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
    ……………………………………………………………….
    Na Daudi Manongi-MAELEZO.
    Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa atafungua maonesho ya Mifuko ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi yatakayofanyika mkoani Dodoma katika viwanja vya mashujaa kuanzia tarehe 18-22 April 2017.
    Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC)  Bi.Beng’i Issa amesema  Maonyesho hayo yameandaliwa na Baraza hilo kwa lengo la kutoa elimu kwa umma juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na mifuko yote ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
    “Tumeamua kufanya maonesho haya kwa mara ya kwanza kwa sababu changamoto kubwa tuliyonayo ni kuwa mifuko hii haifahamiki  sana na wananchi, wengi walikuwa hawajui wafanye nini ili waweze kupata fursa ya kupata mitaji na kusaidiwa na mifuko hii ambayo imeanzishwa na Serikali kwa ajili yao”,Aliongeza Bi.Beng’i.
    Amesema maonyesho hayo yatawapa wananchi fursa ya kuonana na watu ambao wamefanikiwa katika kipindi kilichopita na hasa kujua jinsi gani watafaidika na mikopo ambayo inapatikana kupitia mifuko hii.
    Ameitaja mifuko ambayo  itashiriki ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasiriamali wananchi, Mfuko wa Uwezeshaji wa Mwananchi, Mfuko wa Pembejeo za Kilimo , Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Mfuko wa Dhamana  za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati na Mfuko wa Dhamana za Mikopo kwa Mauzo ya Nje ya Nchi.
    Mifuko mingine ni Mfuko wa kuwasaidia makandarasi,Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,Mfuko wa Misitu Tanzania,SELF Microfinance Fund na PASS Trust Fund.
    Kauli mbiu ya Maonyesho haya ni

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI