Timu ya taifa ya
vijana wa Ghana chini ya miaka 17, wameonyesha wametokea katika nchi ya
soka. Lakini vijana wa Tanzania, Serengeti Boys wakaonyesha wanajua
zaidi kwa kuwa wako katika nchi ya vipaji.
Mechi ya kirafiki ya
kimataifa ya timu hizo mbili imeisha kwa sare ya mabao 2-2 kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.
Ghana walianza kupata mabao yao mapema kupitia Sulley Ibrahim kabla ya Arko Mensah kuongeza la pili.
Hadi dakika za nyongezwa zinaonyeshwa, Serengeti ilikuwa nyuma kwa mabao mawili.
Lakini dakika ya
90+5, mshambuliaji hatari wa Boys, Assad Juma akafunga bao la mkwaju wa
penalti baada ya beki wa Ghana kunawa eneo la hatari.
Dakika ya 90+10, Muhsin Malima akavunja mtego wa kuotea na kumalizia kazi nzuri ya kiungo wao.
Bao hilo liliamisha
shamrashamra uwanjani hapo na ikaonyesha kweli Boys wanastahili
kuchangiwa, wanastahili kuandaliwa ili wakafanye vizuri nchini Gabon
katika michuano ya Kombe la Mataifa Afrika.
No comments:
Post a Comment