• Breaking News

    ..

    ..

    Monday, 3 April 2017

    MASHABIKI WA SIMBA MKOANI GEITA WAJITOKEZA KUIPOKEA TIMU YAO KAMA MFALME


    Q
    Timu ya Simba
    imetua Mkoani Geita  ikitokea Kagera  kwaajili ya kuweka kambi ya siku nne
    kujiandaa na mchezo Dhidi ya Mbao Fc na Toto zote za Jijini Mwanza Mchezo ambayo
    itapigwa kwenye Dimba la CCM Kirumba.

    Ikiwa Mkoani
    Geita Simba inatarajia kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Geita Gold Sport
    Siku ya Jumatano mechi ambayo itachezwa kwenye
    uwanja wa shule ya msingi  Waja.
     
    Kwa Mujibu
    wa Nahodha wa Kikosi cha Simba Jonas Mkude amewataka mashabiki kuendelea
    kuhishabikia timu hiyo na kwamba wataakikisha wanafanya vizuri kwenye
    mchezo  ambayo imebakia.
     
    Hata Hivyo
    kwa upande wake Mussa Hassan Mgosi ameelezea kuwa wamejipanga vizuri kukutana
    na Mbao Fc siku ya Jumatatu na kwamba hawatawaangusha mashabiki wao na ni vyema
    wakasahau ambayo yamepita na  mashabiki
    wakashikamana na timu ili kuweza kutimiza malengo ambayo wamejiwekea

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI