KAMATI
ya Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), imeipokonya Simba ushindi wa mezani waliopewa baada ya kufungwa
na Kagera Sugar 2-1 Aprili 2, mwaka huu Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Kamati
ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa
72 iliipa Simba SC ushindi wa mabao matatu na pointi tatu baada ya
kujiridhisha, beki Mohammed Fakhi aliichezea timu ya Kagera Sugar akiwa
ana kadi tatu za njano.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jioni hii ofisi kwake, Uwanja wa Karume, Ilala
mjini Dar es Salaam, Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema kwamba
Kamati imegundua makosa kadhaa katika maamuzi ya Simba kupewa ushindi wa
mezani.
Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii ofisi kwake, Uwanja wa Karume, Ilala mjini Dar es Salaam
Alisema
kwanza malalamiko ya Simba hayakuwasilishwa ndani ya wakati kwa mujibu
wa kanuni ya 20 kifungu cha kwanza cha kanuni za Ligi Kuu toleo la mwaka
2006 inayotaka malalamiko yote yawasilishwe kwa maandishi Bodi ya Ligi
siyo zaidi ya saa 72 baada ya mchezo kumalizika kwa mchezo.
Akasema
pili malalamiko hayo hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni ya 20
kifungu cha nne kinachosema ada ya malalamiko ni Sh. 300,000 na kwamba
malalamiko yatakayowasilishwa bila kulipiwa ada au baada ya muda
uliowekwa hayatasikilizwa.
Sababu
ya tatu aliyoitaja Mwesigwa ni kwamba kikao cha Kamati ya Usimamizi na
Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa 72 kilikosa
uhalali baada ya kuwashirikisha Wajumbe waalikwa ambao siyo sehemu ya
Kamati hiyo.
“Kwa
maana hiyo matokeo ya mchezo kati ya Kagera Sugar na Simba Sports Club
yanabaki kama yalivyokuwa awali, vile vile Katiba Sheria na Hadhi za
Wachezaji inamuagiza Katibu Mkuu wa TFF kuwapeleka katika kamati za
kinidhamu na Maadili baadhi ya watendaji wa bodi ya ligi kwa
kutokuwajibika katika nafasi zao na kuipotosha Kamati ya Kamati ya
Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania, maarufu kama Kamati ya Saa
72,”amesema Mwesigwa.
Kuhusu Fakhi, Mwesigwa kama alikuwa ana kadi za njano ataitumikia katika mchezo ujao wa timu yake.
Ikumbukwe
Kamati ya Saa 72 iliipa Simba SC pointi tatu na mabao matatu baada ya
kujiridhisha beki wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi aliichezea timu hiyo
dhidi Wekundu wa Msimbazi Aprili 2, mwaka huu akiwa ana kadi tatu za
njano, ambayo ni kinyume cha kanuni.
Lakini
siku mbili baadaye, Kagera Sugar wakapinga maamuzi hayo na kuomba suala
hilo lisikilizwe upya kwa kuwa mchezaji wao hakuwa na kadi tatu za
njano siku wanaifunga Simba 2-0 Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Ndipo
TFF ikaliwasilisha Katiba Sheria na Hadhi za Wachezaji ambayo leo
imemaliza sakata hilo kwa kuirudishia Kagera Sugar pointi zake.
Pamoja
na hayo, Simba inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 59 baada ya
kucheza mechi 27, wakifuatiwa na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi
56 za mechi 25
No comments:
Post a Comment