YANGA
SC leo imezindua utaratibu wa wanachama wake kuichangia klabu kupitia
simu za mikononi ambao utasimamiwa na kampuni ya Selcom ya Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema leo katika mkutano na
Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam kwamba utaratibu huo unaanza
mara moja.
Mkwasa
ambaye ni mchezaji na kocha wa zamani wa Yanga, aliitaja namba ya
kuchangia kuwa ni 150334 ambayo watumiaji wa mitandao yote ya simu za
mkononi wanaweza kuitumia kuchangia klabu yao.
Mkwasa
amesema kwamba wameingia mkataba wa awali wa majaribio na Selcom kwa
miezi mitatu na watakapoona zoezi hilo lina manufaa kwao, wataongeza
mkataba.
“Huu
ni mkataba wa awali tu wa majaribio na tutakapoona zoezi hili
linakwenda vizuri, baso tutakaaa chini na wenzetu kufikiria namna ya
kuongeza,”alisema.
Charles
Boniface Mkwasa (kushoto) akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao
makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam. Kulia ni mwakilishi wa Selcom, Gallus Runyeta
Kwa upande wake, mwakilishi wa Selcom, Gallus Runyeta alisema kwamba wana matumaini zoezi hilo litafanikiwa sana na Yanga watafutahia.
“Sisi
kama Selcom tunafurahi kuingia katika ndoa hii na Yanga ambayo ni klabu
kongwe na wapenzi wengi hapa nchini, na tunawaomba watu wote wenye
mapenzi na Yanga wajitokeze sasa na kuanza kuichangia klabu yao,”alisema
Gallus.
Wakati
huo huo: Mkwasa amesema kwamba kikosi cha Yanga kitaondoka kesho Dar es
Salaam kwenda Dodoma kwa mchezo mmoja wa kirafiki kikiwa njiani
kuelekea Mwanza, ambako Jumapili kitakuwa na mchezo wa mashindano.
Yanga
watamenyana na Kombaini ya Majeshi Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Jumatano, kabla ya Jumapili kuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sporrs Federation (ASFC).
Na
mapema Jumatatu kikosi hicho kinatarajiwa kuendelea Dar es Salaam
kuendelea na maandalizi ya mechi zake za viporo za Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara
No comments:
Post a Comment