• Breaking News

    ..

    ..

    Sunday, 23 April 2017

    taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii kuhusu thamani halisi ya hisa za Vodacom

    Kumekuwa na taarifa za upotoshaji katika mitandao ya kijamii kuhusu thamani halisi ya hisa za Vodacom (VTL). Kwa mfano, ujumbe uliosambazwa tarehe 19 Aprili umedai kuwa bei ya TZS 850 kwa hisa ni mara 3.8 zaidi ya thamani halisi ya hisa hizi. Kufikia hapo, mwandishi alikokotoa thamani ya vitabuni ya rasilimali za kampuni, akatoa dhima (madeni), na kudai kuwa albaki ndiyo thamani halisi ya hisa za wamiliki wote wa kampuni. Njia hii ni potofu, na inaonyesha ni kwa kiwango gani mwandishi haelewi jinsi thamani za hisa na kampuni zinavyo kokotolewa. Kwa mfano, mwandishi anadai kuwa ukweli kwamba bei ya toleo ya hisa za VTL ya TZS 850, sawa na mara 3.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali kujitoa dhima, ni ushahidi kuwa bei imewekwa ya juu sana. Lakini siku hiyo hiyo, bei ya hisa za Safaricom katika siko la hisa la Nairobi ilikuwa ni mara 5.8 ya thamani ya vitabuni ya rasilimali baada ya kutoa dhima

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI