Jumuiya ya Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT) unatoa pongezi kwa Wabunge wa Bunge Tukufu la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kutumia haki yao ya kidemokrasia, kikatiba na
kikanuni kufanikisha uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki uliofanyika
tarehe 4/4/2017 bungeni mjini Dodoma.
Pia unawapongeza Wabunge
waliochaguliwa kuiwakilisha nchi yetu katika Bunge la Afrika Mashariki,
tunawataka kuwa wazalendo, waadilifu, wachapakazi
na wenye kutanguliza maslahi ya nchi yetu Tanzania kwanza.
Pia, UWT imeridhishwa na hatua za mchakato wa uchaguzi huo
ndani ya Bunge na inapongeza demokrasia pana, komavu na shirikishi
iliyooneshwa na wabunge kwa kupiga kura ya HAPANA kwa wagombea
waliotokana na CHADEMA kwa sababu uteuzi wao haukuzingatia misingi ya
demokrasia, uwakilishi wa Kitaifa wala jinsia.na wenye kutanguliza maslahi ya nchi yetu Tanzania kwanza.
Uteuzi uliofanywa na CHADEMA hata
baada ya kushauriwa, unadhihirisha dharau kubwa na kutothamini mchango
wa Wanawake wa Tanzania katika maendeleo ya nchi yetu.
Bunge na Wabunge lazima wawe mstari wa mbele katika juhudi za
kuimarisha demokrasia yetu kama Taifa na ndani ya vyama vya siasa, kamwe
Bunge lisiruhusu kutumika kama “rubber stamp” kama ambavyo CHADEMA
walipanga kwa kuteua wagombea wawili pekee na kwa kufanya hivyo tayari
waliamua nani awe mbunge na kulinyima Bunge fursa na uhuru wa kuchagua
miongoni
mwa wagombea.
Aidha, UWT imesikitishwa sana na kauli za MATUSI, DHARAU na
KEJELI alizozitoa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa
CHADEMA Mhe Freeman Mbowe dhidi ya Wabunge na Bunge Tukufu la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.mwa wagombea.
Kitendo cha Mhe. Mbowe kuwatukana
Wabunge sio tu kinakiuka Kanuni za Maadili ya Viongozi lakini pia
kinatweza UTU na HESHIMA ya wabunge na bunge mbele ya jamii.
UWT inaungana na Maamuzi ya Mhe.
Spika ya Kuwaita watovu wa nidhamu kwenye Kamati ya Maadili.Hata hivyo
tunamtaka Mhe. Freeman Mbowe kuomba radhi wabunge na Umma wa Tanzania
kwa lugha isiyo na staha.
Pamoja na kuomba radhi, tunamtaka
Mhe Mbowe afute kauli yake ya kuwahusisha na kuwatuhumu Viongozi wa
Serikali (Rais na Waziri Mkuu) na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kuwa
wameingilia uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ndani ya
Bunge.
UWT inaendelea kuwahimiza Wabunge kujadili na kupitisha
Bajeti kwa kuzingatia vipaumbele muhimu kwa Maendeleo ya Jamii na Ukuaji
wa Uchumi ikiwemo Ujenzi wa Miundombinu ya Maji, Afya, Elimu, Umeme
Vijijini, pamoja na kuimarisha njia za Uchukuzi na Mawasiliano k.v
Barabara na Reli.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
AMINA MAKILAGI
KATIBU MKUU
UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA {UWT}
05 April, 2017
KATIBU MKUU
UMOJA WA WANAWAKE TANZANIA {UWT}
05 April, 2017
No comments:
Post a Comment