. Madaktari kutoka hospitali ya Aga Khan nchini na Prince Alykhan nchini India wanatarajia kuboresha huduma za upasuaji wa mifupa na majeraha kwa kutumia mtandao wa whatsapp.
Madaktari hao wanatarajiwa kuanza kutumia mbinu hiyo mpya pindi madaktari bingwa kutoka India watakaporudi nchini kwao.
Lengo kubwa ikiwa ni kuendelea kuimarisha na kuendeleza��ushirikiano na kuongeza uwezo wa utoaji huduma kwa wagonjwa.
Akizungumza na waaandishi wa habari jana Daktari bingwa wa upasuaji wa Mifupa na Majeraha kutoka hospitali ya Aga Khan jijini hapa Dk Harry Matoyo alisema licha ya madaktari hao kuondoka na kuwaachia ujuzi mpya mawasiliano kati yao yatakuwa ni ya kudumu.
?Tumetengeneza group (kundi) kwenye whatssap ambalo litatumika na madaktari bingwa wa upasuaji wa mifupa kati ya nchi hizi mbili kwa ajili ya kusaidiana endapo tutakwama kitu Fulani wakati wa kufanya upasuaji tunao uwezo wa kupiga picha na kuuliza kitu gani kinatakiwa kifanyike? alisema Matoyo
Alisema hali hiyo itasaidia kupunguza idadi ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nchini India kwa kutumia pesa nyingi na badala yake watatibiwa nchini.
Pia alisema India ni nchi ambayo imeendelea katika upande wa madawa hivyo kutawaongezea uwezo mkubwa kiutendaji kazi na kupata teknolojia mpya.
?Kuna utaalamu mpya wa kutumia komputa katika kufanya upasuaji kama goti ambalo limeharibika vibaya kuna uwezekano mkubwa wa kulitengeneza upya kwa kutumia teknolojia hiyo lakini kwa kawaida ni jambo lisilo wezekana? alisema Matoyo
Alisema hii italeta faida nchini kwani zitawaongezea uwezo Zaidi wa kutibu wagonjwa na kupunguza idadi ya watu waliokuwa wakienda kutibiwa nchini India.
Daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa(ubadilishaji wa Nyonga bandia na magoti) Dk Julius dinda alisema Tanzania ina Zaidi ya miaka 10 tangu kuanzisha huduma ya upasuaji wa mifupa lakini matatizo yamekuwa yakiongezeka kutokana na uelewa wa watu na wao kutumia mbinu za kizamani.
?Wagonjwa wamekuwa wakiongezeka kutokana na matangazo mbalimbali na elimu inayotolewa kwa wananchi hivyo kufanya hospitali zinazotoa huduma hizo kuelemewa na watu wanaohitaji huduma?, alisema Dinda
Alisema Madaktari hao wataweza kuongezea uwezo uliokuwepo zamani na kuwapa mbinu mpya kutoka nchini kwao ili kuweza kupunguza idadi ya wagonjwa waliokuwa wakikaa kusubiri huduma kwa muda mrefu.
Afisa mtendaji mkuu kutoka Hospitali ya Prince Alykhan, Mumbai, Sanjay Oak alisema licha ya kubadilishana uzoefu na madaktari kutoka nchini pia wataweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa.
?Leo (jana) nitafanya upasuaji wa wagonjwa wawili kutumia njia ya kisasa na kesho Dk. Fahad Shaikh atafanya upasuaji kwa watoto wawili waliopatikana?, alisema Oak.

No comments:
Post a Comment