picha zote na Ahmed Kombo
NA CHRISTINA MWAGALA, OMJ
MEYA
wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo amemtembele mjane wa
aliyekuwa Mhasisi na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema) Bob Makani , Mama Kaboga Makani ikiwa ni moja
ya ziara zake za kutembelea wazee pamoja na viongozi ambao waliwahi
kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Meya
ambaye amerejea Nchini jana kutoka Nchini Iran ambapo alikuwa kwa
ziara ya kikazi ya siku 10, amesema kwamba hatua ya kutembelea
viongozi pamoja na wazee ambao ni waasisi inalenga kutambua michango
yao katika nafasi ambazo waliwahi kutumikia na kwamba busara zao pia
ndio zimeweza kulifikia Taifa sehemu ilipo hivi sasa.
Alifafanua
kuwa Bob Makani enzi za uhai wake alikuwa ni mmoja na mwa sisi wa
Chadema na kwamba anatambua mchango wake kutokana na juhudi
alizozionyesha ikiwemo kukipigania chama hadi kufikia kilipo hivi
sasa.
Alisema
Bob Makani pamoja na wenzake ndio waliokianzisha Chama Cha Chadema na
kufika mbali zaidi kwamba bila wao hata yeye asingekuwa Meya wajiji
hili kupitia chama hicho na kwamba mchango wao ndani ya chama bado
utaendelea kukumbukwa na kila mmoja wakiwemo wanachama wa chama hicho
na wananchi kwa ujumla.
Alisema
Bob Makani mbali na kuwa mwanachama na mwasisi wa Chadema lakini pia
aliwahi kuwa Gavana wa Benki kuu ambapo alitumikia nafasi hiyo kwa na
hivyo baada ya kustaafu nafasi hiyo aliamua kuanzisha chama na hivyo
kuwepo hadi hivi sasa.
“
Haya sio mambo ya kisaisa ,
lakini unaweza kuona kwamba ni alikuwa mtu muhimu , lakini pia kama
kijana wao lazima nipate basara kutoka kwao, ingawaje hatunaye tena
hapa duniani, lakini huko alipo anaona jambo gani ambalo tunafanya
kama vijana ambao alituacha ndani ya chama” alisema.
Alifafanua
kwamba jambo la kutembelea viongozi ama waasisi wa nafasi chama sio
jambo la kisiasa bali ni kutokana na kutambua mchango wakazi ambazo
waliwahi kuzifanya wakati huo.
“
Ziara hii sio ya kwa Mzee
Makani tu, ila ni kwa waasisi , na wale ambao waliwahi kuwa viongozi
wa jiji, wapo nitawatembelea, ikiwa ni sehemu yangu pia ya kutambua
mchango wao, sambamba na kupata baraka , busara zao ambazo
walizitumia katika uongozi wao, ukizungumza vizuri na wazee hawa
unapata baraka na kuona kwamba namna gani unaweza kuwaongoza
wananchi” alisema Meya Mwita.
No comments:
Post a Comment