• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 17 May 2017

    Sheta atoa ahadi kwa Yatiwa


    Kutoa ni moyo na wala sio utajiri. Msanii Shetta ameahidi kuanza kusaidia watoto yatima na watu wasiojiweza.
    Hitmaker huyo wa Namjua, ameahidi kuzunguka mikoa ya Tanzania nzima ili kuweza kuwafikia watu hao katika kipindi cha kuelekea mfungo wa Ramadhan, lakini atafanya hivyo endapo atapata taarifa kutoka kwa watu hao kutokana na mawasiliano ambayo tayari ameyatoa.
    Shetta ametoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa Instagram kwa kuandika:
    Msimu wa Ramadhan unakaribia Mimi kama Shetta na menejimenti Yangu nzima napenda kukufahamisha kuwa kwa kidogo nilichonacho natarajia kuanza kusaidia na kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na wenye uhitaji mkubwa mikoa yote ya Tanzania ambayo nitaweza kuifikia,Naamini Vipo vituo vingi vyenye uhitaji mkubwa sana wa mahitaji ya kila siku. Hivyo basi popote ulipo kama unajua au unahusika na kituo chochote usisite kuwasiliana nasi kupitia;
    Social media( Instagram, Tiwtter, FaceBook; @OfficialShetta or @MxCarter )
    Email; shettamusic@gmail.com or MxCarter@slidevisuals.com
    Simu; +255 22 278 0288 / 0655653030
    Ili tuweze kukufikia kwa Urahisi Kabisa. #ShettaGivesBackToCommunity #RamadhanKareem #MunguWaKwetuSote🙏

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI