Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), akizungumza na Mkuu wa
Wilaya ya Kongwa Bw. Deogratius Ndejembi (kulia), wakati alipokuwa
akikagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa KM 11.71
inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw.
Deogratius Ndejembi (kulia), akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), mara
baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Mbande – Kongwa KM 11.71
inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Sehemu ya barabara ya Mbande – Kongwa yenye urefu wa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma jana.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng.
Salome Kabunda (kushoto), wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa
barabara ya Mbande – Kongwa KM 11.71 inayojengwa kwa kiwango cha lami,
mkoani Dodoma jana
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kongwa
Bw. Deogratius Ndejembi (wa pili kushoto), pamoja na viongozi wengine wa
Serikali wakikagua barabara ya Hogoro – Kongwa KM 14.57 kwa kiwango cha
changarawe wilayani humo, mkoani Dodoma jana.
………………………………………………………………………..
Serikali imesisitiza nia yake ya
kuhakikisha ujenzi wa barabara ya Mbande-Kongwa yenye urefu wa KM 11.71
inayojengwa kwa kiwango cha lami unakamilika kwa wakati.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema hayo mkoani Dodoma jana, mara
baada ya kukagua sehemu ya mradi wa barabara ya Mbande-Kongwa-Mpwapwa
yenye urefu wa KM 49.14 ambao ujenzi wake unaendelea na kumuagiza Kaimu
Meneja Wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng.
Salome Kabunda kusimamia mradi huo kikamilifu.
“Tutahakikisha fedha za mradi huu
zinapatikana kwa wakati ili mradi ukamilike mapema ikiwa ni mkakati wa
kuifungua wilaya hii na kuhuisha fursa za kimaendeleo kwa wananchi wa
Wilaya ya Kongwa na Mpwapwa”, amesema Eng. Ngonyani.
Ameongeza kuwa kukamilika kwa
mradi huo kutafungua fursa za uwezekezaji katika maeneo hayo ikiwemo
kurahisisha huduma za usafirishaji wa mazao kwa Wilaya hizo mkoani humo.
Naye, Kaimu Meneja wa TANROADS,
mkoa wa Dodoma Eng. Kabunda, amemhakikishia Naibu Waziri kuwa
watamsimamia Mkandarasi anayejenga barabara hiyo kwa karibu ili ubora wa
barabara hiyo uendane na thamani ya fedha.
Aidha, Eng. Kabunda amewataka
wananchi wa Wilaya ya Kongwa kushirikiana na mkarandarasi ili kuwezesha
ujenzi huo kwenda kwa haraka.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw.
Deogratius Ndejembi ameishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara
hiyo kwani utachochea maendeleo wilayani humo.
Takribani shilingi Bilioni 7.5
zinatarajiwa kutumika katika sehemu ya kwanza ya mradi huo wa
Mbande-Kongwa ambapo KM 5 zitajengwa na zinatarajiwa kumalizika ndani ya
miezi nane.
No comments:
Post a Comment