Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) akikabidhi
mikataba ya Wazabuni, Mwingine ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Me
Boniface Jacob (Katikati)
Zoezi
la utiliaji saini Mikataba kazi za Manispaa ya Ubungo likiongozwa na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na
Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Me Boniface Jacob (Katikati)
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (mwenye maiki?)
Akizungumza wakati wa kusaini mikataba kazi, Mwingine ni Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob na Naibu Meya wa Manispaa ya
Ubungo Mhe Ramadhan Kwangaya
Zoezi
la utiliaji saini Mikataba kazi za Manispaa ya Ubungo likiongozwa na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) na
Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Me Boniface Jacob (Katikati)
………………………………………………..
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amesaini mikataba ya kazi
mbali mbali na makampuni ya Ujenzi, Barabara na Wazabuni 29.
Mikataba
hiyo imesainiwa mbele ya waandishi wa habari katika dhifa iliyofanyika
katika ukumbi wa Mikutano uliopo Mtaa wa Kibamba CCM, Jijini Dar es
salaam.
Katika
dhifa hiyo iliyohudhuriwa pia na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo
Mhe Boniface Jacob jumla ya mikataba 29 ilisainiwa na wakurugenzi wa
makampuni mbalimbali ambapo kati ya makampuni hayo, Makampuni 14
yamepewa kazi za Billioni 3.2 kwa kazi ya kusafisha barabara na
mazingira yote ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ili kuifanya
Halmashauri ya Ubungo kuwa katika Hali ya usafi.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa tukio hilo la kusaini mikataba Mkurugenzi Kayombo
alisema kuwa mikataba kazi hiyo ipo katika makundi matatu ambayo ni
miradi ya Maji, Barabara na usafi.
‘’Nawasihi
wazabuni wote ambao mtasaini mikataba kazi hapa leo mkatekeleze yale
yaliyo katika mikataba yenu ya kazi mimi kama Mkurugenzi sitasita
kufuata kanuni na taratibu za kisheria na kuwachukulia hatua wale wote
watakaoshindwa kufuata yale ambayo yako katika mikataba yenu’’ . Alisema
Kayombo
MD
Kayombo alisema kuwa katika nakubaliano hayo jumla ya Shillingi
Millioni 400 zimesainiwa kwa ajili ya uchongaji wa barabara za Mitaa
mbalimbali ya Halmashauri na Shilingi Millioni 200 Ni kwa ajili ya
Miradi ya upelekaji wa maji katika kata za Mbezi na Mabibo.
Alieleza
kuwa Kiasi kingine cha shillingi Millioni 200 ni kwa ajili ya Ukarabati
mfumo wa maji Hospitali ya Sinza na ujenzi wa madarasa ya shule ya
Sekondari ya Matosa sambamba na Nyumba sita za walimu zilizopo Kata ya
GOBA.
Naye
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob alisema kuwa
Manispaa ya Ubungo imeingia katika historia kwa kusaini mikataba kazi
hiyo na historia hiyo inatokana na umahiri wa Watumishi wa Manispaa hiyo
katika Kusimamia Ukusanyaji wa Mapato na kubana Matumizi ya ruzuku
zinazotoka Serikali kuu.
“Manispaa
yetu ina miezi nane tu na tayari leo tunasaini mikataba kazi ambayo
italipwa kwa fedha zetu za ndani hili ni jambo la kujivunia sana ‘na
baada ya miezi michache tutasaini tena mikataba kazi mingine na kwa hii
mikataba tunayosaini hapa leo tayari fedha zake zipo kwenye akaunti kwa
hiyo ni suala la utekelezaji tu Alisema Jacob.
Alisema
kuwa anaamini wote wanaosaini Mikataba hiyo hakuna hata mmoja
aliyepenyeza Rushwa au Hongo yoyote na ndio maana mikataba hiyo
imesainiwa kwa Uwazi na Ukweli na hakuna hata siku moja Manispaa ya
Ubungo itasaini Mikataba kwa kujificga au kwenye giza alisisitiza
Mstahiki Boniface Jacob.
Miongoni
mwa mikataba kazi ambayo imesainiwa ni Ukarabati wa Mradi wa Maji
Goba, Ukamilishaji wa ujenzi wa madarasa na vyoo shule ya Sekondari
Luguluni katika kata ya Kwembe, Ukamilishaji wa Ujenzi wa Madarasa ya
shule ya Sekondari Matosa.
Pia
ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba za walimu (6 in 1) katika Sekondari ya
Matosa, Matengenezo ya Barabara ya Watani Makaburini (Makurumla),
ujenzi na ukarabati wa mfumo wa maji katika hospitali ya Sinza, Ujenzi
wa kivuko cha Mabibo katika Manispaa ya Ubungo, kutoboa na kuweka maji
katika Barabara ya Sam Mujoma na Mandela Manispaa ya Ubungo, Mradi wa
maji Mbezi Luiz na Ukarabati wa mradi wa Maji Mabibo Jeshini, Mabibo na
Kawawa.
Akizungumza
kwa niaba ya wazabuni wenzake, mzabuni wa Kampuni ya Singaruki
Investment Ltd alisema kuwa kampuni zote zilizopata kazi katika Manispaa
ya Ubungo ni dhahiri kuwa zilistahili kutokana na ufanisi katika
utendaji kazi.
Alisema
tayari wameshasaini mkataba kazi hivyo jambo la msingi ni kutekeleza
yale yote yaliyopo katika mikataba kazi kwa kufuata kanuni na taratibu
za kisheria ambazo zimeainishwa kwenye Mikataba.
Aidha
Mkurugenzi Kayombo ametoa siku 14 kwa wakandarasi wote kuhakikisha
wanarudisha mikataba ya makubaliano mara baada ya kuisoma na kuielewa
sambamba na kujaza mikataba hiyo.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
No comments:
Post a Comment