Taasisi inayojishughulisha na utetezi wa maswala ya Elimu ( HAKI ELIMU) imezindua kampeni maalum yenye lengo la kukabiliana na changamoto za kimazingira, kiuchumi na zakimazoea ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma haki ya upatikanaji wa elimu bora kwa mtoto wa kike Nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari Mapema leo hii Jijini hapa Mkurugenzi Mtendaji wa haki Elimu John Kalege amesema kampeni hii inachangiwa na ukweli kuwa,elimu ya mtoto wa kike inachangamoto mbali mbali ambazo hazina budi kutatuliwa ilikuwawezesha watoto wa kike kuwa shuleni na kupata elimu bora inayomwezesha kutimiza ndoto zao hasa katika kuendeleza maisha yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema ya watoto wa kike siti na tisa elfu kwa mwaka 2015 walikosa masomo kutokana changamoto mbali mbali ikiwemo mimba, utoro na vifo.
Sanja na hayo amesema kuwa uwiano kwa wavulana na wasichana elimu ya msingi ni 1:1 hali ni tofauti katika elimu ya kidato cha tano na sita kwani ni ndogo ikilinganishwa na wavulana ambapo uwiano ni 1:2 ambapo wavulana ni mara mbili ya wasichana .
Hatahivyo ameongeza kuwa serekali inatakiwa kuhakikisha kuwa inatekeleza kwa vitendo wajibu wake wa kuhakikisha watoto wote wanapata elimu bila ubaguzi wa aina yeyote ikiwemo kutatua changamoto za mazingira ya kujifunzia na kufundisha na kufanikisha kuwepo kwa elimu jumuishi katika elimusingi.
..
Tuesday, 20 June 2017
Habari
No comments:
Post a Comment