Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Wazazi Zanzibar , Mustafa Rashid Kumwalu akimkabidhi Katibu wa Wazazi
Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja , Bi. Salma Shaibu, kwa niaba ya Naibu
Katibu Mkuu wa Umoja huo Bi.Najma Giga.
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa
Wazazi Zanzibar Nd. Mustafa Rashid Kumwala akitoa nasaha kwa Makatibu
wa Wilaya Sita za Umoja huo kabla ya kuwakabidhi komputa hizo.
Baadhi ya Komputa zilizotolewa na
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Zanzibar, Bi.Najma Giga kwa Wilaya
Sita za umoja huo Zanzibar.
……………………………………………………………………..
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKATIBU wa Wilaya za Umoja wa
Wazazi CCM Zanzibar wamewashauri viongozi mbali mbali wa Chama cha
Mapinduzi kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi walizotoa ndani ya
taasisi hiyo ili kupunguza changamoto za kiutendaji.
Rai hiyo imetolewa na baadhi ya
Makatibu wa Wilaya Sita za Umoja huo Zanzibar mara baada ya kukabidhiwa
Komputa zilizotolelewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bi. Najma Giga
ikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa ahadi alizowahi kutoa wakati wa
ziara zake Visiwani humo.
Katibu wa Wazazi Wilaya ya
Amani , Bi.Mwanaisha Ame Mohamed amesema upatikanaji wa vifaa hivyo
utaongeza ufanisi wa kiutendaji ndani ya umoja huo kwani watakuwa na
vitendendea kazi vya kisasa vitakavyorahisisha utendaji wa kazi zao.
Aidha Katibu huyo amewataka
baadhi ya Wabunge, Wawakilishi na Madiwani ambao bado hawajahamasika
kuanza kutekeleza ahadi zao kwa umoja huo na chama kwa ujumla kufuata
nyayo za viongozi wenzao walioanza kutatua kero za taasisi hiyo hatua
kwa hatua.
“Huu ni wakati wa viongozi mbali
mbali wa Chama chetu pamoja na jumuiya zetu kujitokeza kusaidia baadhi
ya Mikoa na Wilaya zenye upungufu wa vitendea kazi ili waweze
kukamilisha shughuli za uchaguzi kwa ufanisi.”, alisema Katibu
Mwanaisha.
Naye Katibu wa Wazazi Wilaya ya
Wete Pemba, Bi. Mariam Ali Said amemshukru Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi
Zanzibar kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo na kuongeza kuwa vifaa
hivyo ni chachu ya kumaliza changamoto za kufuata huduma za uchapaji
wa nyaraka za kiofisi masafa ya mbali.
Akizungumza Kaimu Naibu Katibu
Mkuu Wazazi Zanzibar, Nd. Mustafa Rashid Kumwalu kwa niaba ya Naibu
Katibu Mkuu wa umoja huo Bi. Najma Gina mara baada ya kukabidhi
Komputa hizo ametoa wito kwa watendaji wa umoja huo kutumia komputa
hizo kwa matumizi yaliyokusudiwa ili shughuli za kiutendaji zifanyike
kwa wakati mwafaka.
Nd. Rashid alieleza kuwa lengo
la umoja huo ni kuhakikisha watendaji wake wanapata vitendea kazi vya
kisasa vitakavyosaidia kutekeleza kwa wakati shughuli za kiutendaji
kwa lengo la kwenda sambamba na matakwa ya Katiba ya CCM iliyofanyiwa
mabadiliko miezi kadhaa iliyopita.
Aidha alisema Komputa
zilizokabidhiwa mpaka sasa ni tisa bado kumi kwa mujibu wa idadi ya
komputa zilizoahidiwa kutolewa na Naibu katibu Mkuu wa Umoja huo, ambaye
pia ni Mbunge wa kuteuliwa kutoka ndani ya Umoja wa Wazazi Tanzania.
Komputa hizo zina thamani zaidi
ya shilingi milioni Saba zimekabidhiwa kwa Wilaya 6 za Umoja wa
Wazazi CCM Wilaya ya Amani, Wilaya ya Mfenesini, Wilaya ya Kati,
Wilaya ya Kaskazini “B”, Wilaya ya Wete na Wilaya ya Chake Chake Pemba.
No comments:
Post a Comment