• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 14 June 2017

    KAMOG:WATANZANIA WANAPASWA KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWENYE KULINDA RASILIMALI ZA NCHI



    unnamed
    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara,
    Hudson Starnley Kamoga akimkabidhi shilingi 150,000 Mwenyekiti wa
    chama cha albino Mkoani humo Joseph Masasi, kwa ajili ya kuwanunulia
    kofia ya kukinga jua kwa watoto wa kituo cha 4 Angel mji mdogo wa
    Haydom.Picha namba mbili.
    1
    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara,
    Hudson Starnley Kamoga, (katikati mwenye miwani) ambaye alikuwa mgeni
    rasmi katika maadhimisho ya siku ya albino duniani kwa niaba ya Mkuu
    wa Mkoa huo akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na
    watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambayo kimkoa ilifanyika Mji
    mdogo wa Haydom wilayani Mbulu.
    2
    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara,
    Hudson Starnley Kamoga akiwa amempakata mtoto mwenye ualbino wa kituo
    cha 4 Angel kwenye maadhimisho ya siku ya albino duniani ambayo kimkoa
    imefanyika wilayani Mbulu.
    ………………….
    Watanzania wametakiwa kumuunga mkono Rais John Magufuli kwenye vita ya
    kulinda rasilimali za nchi aliyoianzisha kwani kwa muda mrefu watu
    wachache walishiriki kufuja mali za nchi ambazo zingetumika kwa
    manufaa ya watu wengi.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkonia Manyara,
    Hudson Starney Kamoga aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya
    albino duniani, ambayo kimkoa ilifanyika kituo cha 4 Angle mji mdogo
    wa Haydom, alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo Dk Joel
    Nkaya Bendera.
    Alisema vita ya kulinda rasilimali ya nchi inapaswa kuungwa mkono
    kwani utajiri wa nchi ya Tanzania haulingani na hali halisi iliyopo
    kutokana na watu wachache kupora utajiri kupitia madini mbalimbali.
    Alisema ana imani Rais Magufuli na watanzania kwa ujumla watashinda
    vita ya kulinda rasilimali kwani kupitia ripoti ya pili ya makania
    imeonyesha namna wananchi wanyonge wanavyoibiwa.
    “Pamoja na kuathimisha siku ya albino duniani tunapaswa kumuunga mkono
    Rais Magufuli katika vita hii ya kusimamia na kulinda rasilimali za
    nchi kupitia madini yetu kwani nia ya dhati ameionyesha,” alisema
    Kamoga.
    Alisema aliwaagiza watumishi wa halmashauri hiyo waangalie kwenye
    runinga na yeye mwenyewe aliiangalia ripoti hiyo kwa lengo la kumuunga
    mkono Rais Magufuli katika kusimamia rasilimali zilizopo kwenye eneo
    hilo.
    “Ukiisikiliza kwa makini hiyo taarifa ya pili ya makinikia na sisi
    ambao tunafanya kazi ya kumsaidia Rais kutimiza ndoto yake ya
    kuhakikisha kuwa wananchi wanyonge wanafaidika na rasilimali
    waliyonayo unaweza ukalia kwa sababu hali iliyopo ni tofauti na
    uhalisia,” alisema Kamoga.
    Alisema wananchi na viongozi wanapaswa kuunga mkono jitihada za Rais
    Magufuli na endapo dhamira ya dhati itakuwepo kwa wote rasilimali za
    nchi zitawanufaisha wananchi wote.
    Naye, Mwenyekiti wa chama cha maalbino mkoani Manyara, Joseph Masasi
    alisema wanakabiliwa na changamoto ya kutobaini idadi kamili ya watu
    wenye ualbino mkoani humo hivyo kukosa takwimu sahihi.
    Masasi alisema tatizo hilo linasababisha hata kukitokea tatizo lolote
    linalohitaji msaada kwao inakuwa vigumu kwani wengine wanakosa
    kutokana na kutobainishwa kwa idadi yao katika wilaya za mkoa huo.
    Alisema pia wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa mafuta maalum ya
    kujipaka kwa watu wenye ualbino yanayowasaidia kila siku ili
    wasiathiriwe na mionzi ya jua na kusababisha baadhi yao kuathirika.
    “Pamoja na hayo tunashukuru kwenye mkoa wa Manyara hakuna matukio ya
    watu wenye ualbino kuuawa au kukatwa viungo na watu makatili ila kuna
    badhi ya matishio madogo madogo,” alisema Masasi.
    Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Joseph
    Mandoo halmashauri yao itaendelea kushirikiana na uongozi wa ualbino
    kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa msaada unaohitajika kwa watu hao.
    Mandoo alitoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ualbino
    kutowafisha ndani na badala yake wawafikishe kwenye sehemu husika ili
    pindi misaada itakapotolewa waweze kupatiwa

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI