Picha ya pamoja ya Wadau wa
Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ikiongozwa na Mganga Mkuu wa
Serikali Prof Bakar Kambi katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya shughuli
za mpango wa Taifa wa magonjwa hayo uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es
salaam.
Wadau kutoka nchi mbali mbali
wakifuatilia mjadala kwa ukaribu katika mkutano wa mwaka wa mapitio ya
shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi
kipaumbele uliofunguliwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar Kambi
(Hayupo kwenye Picha) uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakar
Kambi akiwasirisha mchango wake mbele ya wadau wa magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele (Hawako kwenye picha) katika mkutano wa mwaka wa
mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa wa udhibiti wa magonjwa hayo
uliyofanyika Kunduchi jijini Dar Es salaam.
Mratibu wa Mpango wa taifa wa
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt Upendo Mwingira akifuatilia
kwa ukaribu mjadala uliokuwa ukiwasilishwa na Mganga Mkuu wa Serikali
Prof Bakar kambi (hayupo kwenye picha) katika mkutano wa mwaka wa
mapitio ya shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa
hayapewi kipaumbele, anaefuatia ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya TAMISEMI
Dkt. Ntuli Kapologwe na mkurugenzi wa kinga Dkt Neema Ruzibamayila.
……………………
NA WAMJW DAR ES SALAAM
SERIKALI imejidhatiti kutokomeza
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ili kutimiza malengo ya kujenga
uchumi wa viwanda na afya bora mpaka kufikia 2020.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Mohammed Kambi wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa
mwaka unaolenga kupitia shughuli za mpango wa Taifa wa kudhibiti
magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
“Tunataka mpaka kufikia 2020 tuwe
tumetokomeza magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kama mabusha na
matende ili kuweza kuinusuru nchi katika aina hii ya magonjwa
yanayojitokeza katika nchi zinazoendelea hususan Tanzania” alisema Prof.
Kambi.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa
licha ya kudhibiti mabusha na matende pia wamejidhatiti kuzuia ugonjwa
wa usubi na kichocho kabla ya kufikia 2025 ili kuendana na mpango wa
dunia wa kudhibiti magonjwa hayo.
Kwa upande wake Mratibu wa Mpango
wa Taifa Wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Dkt.
Upendo Mwingira amesema kuwa wananchi wanatakiwa wajitokeze kupata dawa
na tiba za magonjwa hayo kwan hazina madhara kwa binadamu.
Mkutano huo uliokutanisha wadau
mbalimbali wa sekta ya afya kutoka duniani kote umelenga kupata mpango
kazi wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa mwaka 2017
na 2018 ili kuweza kupata njia za kudhibiti magonjwa hayo kama vile
mabusha na matende, kichocho na usubi
No comments:
Post a Comment