NAHODHA
wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti
Boys Issa Abdi Makamba ameshukuru kwa huduma anazoendelea kupatiwa na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati huu akiwa majeruhi.
Makamba
aliumia kwenye kambi ya mazoezi ya Serengeti Boys nchini Morocco mwezi
Aprili kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana
chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon Mei.
Lakini
alikwenda kwenye kambi ya Cameroon na baadaye kwenye fainali za AFCON
U-17 nchini Gabon, ambako Serengeti Boys ilitolewa hatua ya makundi.
Issa Makamba akiwa na wadogo zake nyumbani kwao Dodoma ambako anaishi
Issa Abdi Makamba akiwa mazoezini na Serengeti Boys kabla ya kuumia
Kufuatia kurejea nyumbani, kukaibuka habari kwamba Nahodha huyo ametelekezwa na TFF, jambo ambalo leo amekana.
“Ninapata
simu nyingi sana juu yangu kuwa nimetelekezwa na TFF na kuna taarifa
nying sana zinaenea kuhusu mimi. Ukweli ni kwamba, hapana mimi
sijatelekezwa na TFF,” amesema Makamba.
“Na
kuhusu suala la kwenda Dodoma ni kwetu na wazazi wangu ndiyo
wanapoishi, hivyo kwenda kuwasalimia wazazi wangu imekuwa chanzo cha
vitu vyote hivi. Mimi nipo sawa na ninaendelea vizuri sana tu,”amesema.
Kwa
ujumla wachezaji wote wa Serengeti Boys wapo chini ya uangalizi mzuri
wa TFF baada ya fainali za Gabon kwa sababu wanaandaliwa kuwa timu ya
taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes


No comments:
Post a Comment