Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri amesema kuwa atawachukulia hatua
ikiwemo kuwapeleka katika Mamlaka zao za uteuzi viongozi na Madiwani
ambao wamekuwa wakijitokeza kuwatetea watumishi waliosimamishwa au
kufukuzwa kwa makosa mbalimbali kama vile ubadhirifu wa mali za umma .
Bw.
Mwanri alitoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya siku nne ya
Madiwani na Watendaji wa Manispaa ya Tabora yaliyofanyika wilayani Nzega
kuhusu
jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi jamii ya fursa na vikwazo
kwa maendeleo (O&OD) iliyoboreshwa na usimamizi wa fedha za miradi
ya maendeleo (LGDG)
Alisema
kuwa imekuwa ikijitokeza katika baadhi ya maeneo mtumishi anakuwa
ametuhumiwa kwa makosa mbalimbali na kusimamishwa ili kupisha uchunguzi
tuhuma zake kunajitokeza baadhi ya madiwani au viongozi kujifanya wao
ni watetezi wake bila kujali hasara iliyotokana na utendaji wake na
utovu wa nidhamu.
Bw.
Mwanri alisema hali hiyo imekuwa ikijitokeza katika baadhi ya
Halmashauri kwa sababu ya baadhi ya Madiwani au viongozi fulani kuwa na
maslahi binafsi na mtuhumiwa kwa sababu wanaona kuwa kutokuwepo kwake ni
pigo kwao.
Alisisitiza
kuwa somo la wajibu na maadili walilofundishwa linawataka kuhakikisha
kuwa wanakuwa wazalendo kwa kulinda maslahi ya wananchi na sio kikundi
fulani cha waharifu au wezi.
“Nikimsikia
mtu anamtetea mtumishi aliyefukuzwa au kusimamishwa kwa utovu wa
nidhamu naanza nay eye kama yuko katika uwezo wangu nitamdoa na yeye
ili akamtetee vizuri akiwa nje …na kama ni Diwani nitampeleka katika
Chama chake kwa kuwa ndio kilichompa dhamana ya kwenda kwa wananchi
kuomba kura ili aweze kuchukuliwa hatua kwa sababu ya kuwasaliti
wananchi waliomchagua” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aliwataka
Madiwani wawe na uchungu na wananchi kwanza na kuacha kutetea maovu
katika Halmashauri zao kama wanahitaji maendeleo ya watu wao yaonekana
na majina yao yawekwe kwenye Historia nzuri na sio ile ya kudharauliwa
hata na vijana wadogo.
Naye
Afisa Utumishi , Ofisi ya Rais-TAMISEMI Debora Mkemwa akitoa mada
kuhusu nidhamu kwa watumishi na mashauri ya nidhamu kwa Watumishi wa
Serikali za Mitaa alisema kuwa uchunguzi wa awali unafanyika kabla ya
hatua za kinadhamu kwa mtumishi hazijachukuliwa ili kujiridhisha iwapo zipo sababu za msingi za kuanzishwa mchakato huo.
No comments:
Post a Comment