Imeelezwa
kuwa mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya
kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting
System – FFARS) utasaidia kuondoa malalamiko kwa wanasiasa kuzinyooshea
halmashauri kuwa zinatumia vibaya mali za umma.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa June 9,2017 na
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI), Elisa Rwamiago,wakati wa kufunga mafunzo ya siku
mbili kuhusu mfumo wa FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi
katika vituo vya afya kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala wilaya ya
Kahama mkoa wa Shinyanga,yaliyofanyika katika ukumbi wa Submarine Hotel
mjini Kahama.
Rwamiago alisema wanasiasa wengi
wamekuwa wakizitupia lawama halmashauri za wilaya kutumia vibaya pesa za
serikali kutokana na kukosekana kwa uwazi na mfumo mzuri wa
ukusanyasaji na utunzaji wa taarifa za fedha.
Alisema FFARS itasaidia katika
kufuatilia matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali katika kufikia
malengo ya utoaji huduma na kuhakisha yanaendana na sheria ya manunuzi
na utoaji taarifa, ili kuisaidia serikali kuimarisha mfumo wa usimamizi
wa fedha za umma katika vituo vya kutolea huduma ikiwemo shule,vituo vya
afya na hospitali za wilaya.
“FFARS ina faida kubwa kwetu kwani
kukosekana kwa uwazi ilikuwa ni chanzo cha wanasiasa kusema katika
halmashauri kuna mchwa hivyo mfumo huu utatutoa katika matumizi bubu ya
fedha na kuwa ya wazi zaidi na tunategemea matokeo mazuri”,aliongeza Ramiago.
Naye Mhasibu wa Chuo cha Serikali za
Mitaa Hombolo- Dodoma Bwanakheri Abdi Muhoma anayefanya kazi na mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems
Strengthening – PS3’,alisema pesa za serikali zilikuwa zinatumika vibaya
kutokana na kukosekana kwa mfumo unaofanana katika kukusanya na kuandaa
taarifa za kifedha.
“Huu mfumo utasaidia sana kuongeza uwazi
katika masuala ya fedha kwani pesa za serikali zilikuwa zinatumika
kwenye matumizi yasiyo sahihi hivyo uwajibikaji utakuwepo kwa watendaji
wa serikali”,alieleza Muhoma.
Kwa upande wake Mshauri wa Kifedha
kutoka PS3,Osoro Otieno aliwataka maafisa elimu kata na waganga
wafawidhi katika vituo vya afya walioshiriki mafunzo hayo kutoa elimu
kwa watoa huduma wengine katika shule na vituo vya afya kwani FFARS
inaanza kutumika kuanzia Julai 1,2017.
Nao washiriki wa mafunzo hayo
waliipongeza serikali kuruhusu mfumo huo utumike ili kuongeza
uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya pesa za serikali.
FFARS inatekelezwa na mradi wa
Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems
Strengthening – PS3’,Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and
System Strengthening – (HPSS) unaofadhiliwa na watu wa Uswizi (Swiss
Tropical and Public Health Institute) na TAMISEMI kwa ufadhili wa
Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAFUNZO YA FFARS HALMASHAURI YA MSALALA
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi
kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Elisa Rwamiago
akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa
FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya
kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama
Afisa Msimamizi wa Fedha Mwandamizi kutoka Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Elisa Rwamiago,akizungumza ukumbini
Mshauri wa Kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo
Mshauri wa Mifumo ya Kifedha kutoka PS3,Martin Lawi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo
Afisa Elimu Kata ya Chela,Matunda Hamza akichagia hoja wakati wa mafunzo kuhusu FFARS
Mshauri wa Mifumo ya Utawala Bora ma
Ushirikishwaji wa Wananchi kutoka PS3,Dk. Chinuno Charles Magoti
akiandika dondoo muhimu za mafunzo kuhusu FFARS kwa kutumia kompyuta
Wakufunzi wa mafunzo kuhusu FFARS wakiwa ukumbini
Mshauri wa Mifumo ya Kifedha kutoka
PS3,Martin Lawi akitoa mwongozo kwa mshiriki wa mafunzo hayo kuhusu
namna ya kujaza taarifa za masuala ya fedha
Washiriki wa mafunzo hayo wakichukua
vitendea kazi kwa ajili ya kufundishia kwenye vituo vya kutolea huduma
ikiwemo shule na vituo vya afya katika kata zao
Kulia ni Afisa Elimu kata ya Kashishi
Ally Shaban Misana akipokea fomu kwa ajili kutolea mafunzo katika vituo
vya kutolea huduma kwenye kata yake kutoka kwa Mhasibu wa Chuo cha
Serikali za Mitaa Hombolo- Dodoma Bwanakheri Abdi Muhoma anayefanya kazi
na PS3’.
Zoezi la kugawa vitendea kazi likiendelea
Mratibu wa HPSS halmashauri ya Msalala,Happiness Josephat akijiandaa kugawa vifaa vya kufundishia kwa washiriki wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa na vifaa vya kufundishia kuhusu FFARS kwenye vituo vya kutolea huduma katika kata zao
No comments:
Post a Comment