• Breaking News

    ..

    ..

    Saturday, 10 June 2017

    VIONGOZI WA MASHIRIKA YA UMMA NA BINAFSI WAMETAKIWA KUPIMA AFYA ZAO MARA KWA MARA

    Na Mwandishi wetu – JKCI
    Viongozi wa mashirika ya Umma na Binafsi  wametakiwa kujenga mazoea ya kupima afya zao mara kwa mara ili kufahamu  kama wana magonjwa yanayowasumbua au la na kwa kufanya hivyo wataweza  kupata matibabu kwa wakati.
    Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akiongea na viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya upimaji wa Afya zao.
    0002
    Prof. Janabi alisema baadhi ya viongozi  hawana mazoea ya kupima afya zao japo mara moja kwa mwaka na inapotokea wamegundulika  kuwa na tatizo  la ugonjwa huwa ni  kubwa na limeshaleta madhara mwilini,   na wakati  mwingine huwa  ni vigumu kutibika lakini  tatizo kama hilo likigundulika  mapema katika hatua ya awali  huwa ni  rahisi kutibika.
    Akizungumzia kuhusu magonjwa ya Moyo Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema ni muhimu mgonjwa afuate maelekezo ya jinsi ya kutumia dawa aliyopewa na daktari wake kwani kuna baadhi ya wagonjwa wamekuwa na tabia ya kuacha kutumia dawa pindi wanapojiona wamepata naafuu jambo ambalo siyo sahihi.
     
    Akielezea  jinsi ya kujikinga na magonjwa ya Moyo kwa upande wa chakula Afisa Lishe kutoka JKCI Louisa Shem  alisema ni muhimu kupunguza utumiaji wa vyakula vya mafuta kupita kiasi hasa mafuta yatokananyo na wanyama, kutumia vyakula vya nafaka zisizokobolewa.
    Kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji wa bidhaa zitokanazo na tumbaku ikiwemo sigara, kufanya mazoezi ya mwili angalau nusu saa kwa siku na kupunguza matumizi ya vyakula vyenye chumvi nyingi.
    Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Afya na Usalama Kazini kutoka  NHC Dkt. Yothan Mackenzie  alisema hivi karibuni walikuwa na mkutano wa Baraza la Wafanyakazi katika mkutano huo kulikuwa na mada ya ulaji na afya wakaona ni vyema mada hiyo iende sambamba na upimaji wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa Moyo.
    Dr. Mackenzie alisema wanawapima viongozi hao kwa awamu hadi sasa jumla ya wakurugenzi na wakuu wa vitengo 14 wamepima na kujuwa afya zao na viongozi wengine wataendelea kupima kwani Shirika lao linaamini kuwa  mfanyakazi akiwa na afya njema ataweza kufanya kazi zake vizuri.
    Baadhi ya magonjwa waliyopima viongozi hao ni pamoja na  Moyo, tezi dume, figo na sukari

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI