• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 7 June 2017

    WAZIRI MKUU MAJALIWA ;SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MIFUMO YA ELIMU KWA WATU WOTE

     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Vifaa vya kufundishia kwa watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko Ilala jijini Dar es Salaam.
    Na Humphrey
    Shao, Globu ya Jamii
    Waziri mkuu
    wa Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali imejipanga kuboresha Elimu nchini kwa
    kuongeza bajeti ikiwemo ununuzi wa vifaa na walimu katika shule zenye mahitaji
    maalum.
    Waziri Mkuu
    Majaliwa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua na kukabidhi
    vifaa vya elimu vya kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum nchini
    vyenye thamani ya bilioni sita kutoka shirika la Global Partner ship.
     
    “Vifaa hivi
    vitakwenda katika mikoa yote 26 nchini kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji
    maalum ambapo itanufaisha shule za Msingi 213 kati ya shule 408 na sekondari 22
    kati ya shule 43 zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum” amesema Waziri Mkuu
    Majaliwa .
     
    Amesema kuwa
    pia serikali imenunua vifaa vya kufundishia kwa walimu wanaofundisha watoto
    wenye mahitaji maalum ikiwa ni kielelezo cha kutimiza ahadi za Rais John Pombe Magufuli
    kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata elimu bila ya kujali mapungufu yake.
    Amesema mapungufu
    ya kimwili kiakili sio mwisho wa kufikia malengo kwa watoto wetu kwani bado
    wapo watumishi serikalini ambao wanamahitaji maalum na bado wanafanya vizuri
    katika kazi zao.
     
    Waziri mkuu
    Majaliwa amesema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya walimu na kutoa
    mafunzo ya kitaaluma hili waweze kuendana na mabadiliko ya mitaala nchini.
     
    Wizara
    iakikishe inasimamia na kuwachukulia hatua
    wazazi wote ambao wanaficha watoto wenye mahitaji maalumu na kushindwa
    kwenda shule na kumuagiza waziri wa tamisemi atoe waraka katika Halmashauri
    ziweze kuwahudumia watotoambao wapo kwenye shule za kawaida hili waweze
    kupatiwa vifaa.
    Ametoa wito
    kwa watoto Wazazi na walimu kuwa na nidhamu ya hali ya juu hili kuleta
    umaana  wa vifaa hivi.

     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na viongozi wengine waandamizi wa serikali na wawakilishi wa mashirika yaliyofafadhili vifaa hivyo wakikata utempe kuashiria uzinduzi wa vifaa vya watoto wenye mahitaji Maalum
     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia namna vifaa hivyo vinavyofanya kazi kwa mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko
     Waziri Mkuu Kassim majaliwa akipunga mkono kuwasalimia watu waliofika katika shrehe hizo za uzinduzi wa vifaa vya kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalum.
     Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akitoa Salaam za Mkoa wa Dar es Salaam akimwakilisha RC .Paul Makonda katika hafla hiyo ya uzinduzi wa vifa avya kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum
     Waziri Mkuu Kassim majaliwa akisalimiana na Naibu Meya wa Ilala , Omary Kumbilamotowakati akiwasili katika shule ya msingi Uhuru Mchanganyiko
     Waziri Mkuu Kassim majaliwa akisalimiana na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam ,Saad Kusirawe wakati akiwasili katika shule ya Msingi uhuru Mchanganyiko
     Wanafunzi wa shule ya Msingi umoja wakitoa burudani ya Makirikiri
     Wanafunzi wa uhuru Mchanganyiko wakitoa burudani mbele ya waziri mkuu

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI