• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 7 June 2017

    WORLD MERIT TANZANIA YAJIPANGA KUMRUDISHA RAIS TRUMP KATIKA MABADILIKO YA TABIA NCHI

    Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akimpongeza Kiongozi wa World Merit Tanzania , Rose Mmbaga  katika siku ya kilele cha Mazingira Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.




    Na Humphrey
    Shao, Globu ya Jamii
     
    Tasisi isiyo
    ya Kiserikali inayojiusisha na utunzaji wa Mazingira nchini ya Word Merit
    Tanzania  imesema ipo katika kampeni
    maalum ya kuhakikisha kuwa Rais wa Marekani Donald Trump anatambua uwepo wa
    mabadiliko ya tabia nchi Duniani kwa kuanzisha kampeni ya GREEN TRUMP.
     
    Hayo
    yamesemwa kiongozi wa shirika hilo nchini Tanzania , Rose Mmbaga alipokuwa
    akizungumza na Ripota wa globu ya Jamii wakati wakufunga siku ya Mazingira
    Duniani iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam jana.
     
    “kwa sasa
    tumeamua kuwa na kampeni moja ambayo inakwenda kwa jina la ‘GREEN TRUMP’ Ambayo
    itawakutanisha vijana wanaojitolea kwa kupanda miti nchi nzima hili waweze
    kumuaminisha Rais wa Marekani kuwa mapinduzi ya kijani yanawezekana  licha ya kiongozi huyu kujitoa katika ule
    mkataba wa Paris” amesema Mmbaga.
     
    Ameongeza kuwa
    yeye kama kiongozi kijana ameamua kujikita katika kuhamasisha swala la
    mazingira hili aweze kusaidia vijana wengine kuingia katika mapambano haya hili
    nchi yetu iweze kujikinga na majanga mbalimbali.
    Amesema kuwa
    mabadiliko ya tabia nchi yamekuwa yakileta majanga mengi sana nchini ikiwemo suala
    kurudisha maendeleo nyuma kwa kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa gharama
    kubwa kutoka katika fedha za watanzania.
     
    Alimaliza kwa
    kusema kuwa ufike wakati wa Vijana sasa kutambua na kuheshimu mazingira hili
    yaweze kututunza kwa ajili ya kizazi chetu cha baadae.
    Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akiwa katika picha yapamoja na Vijana wa World Merit Tanzania ambao wamejitolea kutunza Mazingira nchini

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI