Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubia waandishi
nwa habari (Hawapo kwenye picha) katika kilele cha maazimisho ya siku
ya Homa ya Ini Duniani yaliyofanyika leo katika ofisi ndogo za Wizara ya
Afya jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Pro
Muhamad Bakari kambi na Kulia ni Afisa kutoka kitengo cha magonjwa ya
Mlipuko Dkt. Azma Simba.
Waandishi wa habari kutoka vyombo
tofauti wakifuatilia kwa ukaribu tamko la kilele cha maadhimisho ya
Homa ya Ini Duniani lililotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (Hayupo kwenye picha) leo
katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akijadiliana kwa ukaribu
na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Muhamad Bakari Kambi wakati akitoa
tamko kuhusu Homa ya Ini Duniani katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya
jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakifuatilia kwa
umakini tamko lilitolewa na Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha)
katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Homa ya Ini Duniani mapema leo
katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya jijini Dar es salaam.
……………………………..
NA WAMJW –DAR ES SALAAM.
CHANJO ya homa ya Ini inatarajiwa
kupatikana kwa wananchi wote bila kujali kigezo cha umri wala uwezo wa
kifedha kwa wananchi wenye hatari au ugonjwa wa ini kwa bei nafuu mpaka
kufikia mwaka 2020 kutoka mwaka wa fedha 2018/2019.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa
afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu
maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani.
“Katika kuadhimisha siku ya
ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria kuhakikisha chanjo ya
ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao wana hatari ya kupata
maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata ugonjwa huo kwa bei nafuu
kwa mswaka wa bajeti 2018/2019” alisema Waziri Ummy.
Aidha waziri Ummy amesema kuwa
chanjo ya homa ya Ini kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano
inapatikana hapa nchini kwenye vituo vya huduma ya afya vya Serikali na
watu binafsi.
Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema
kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa
damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji
kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu.
Waziri Ummy ameongeza kuwa ugonjwa
wa homa ya ini unaua idadi kubwa ya watu duniani kwa taratibu ikiwa
katika watu 100 watu 8 wana maambukizi ya ugonjwa huo na kutoonyesha
dalili mapema.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
asilimia 50 ya wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano wana
maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini hivyo kuwataka watanzania
kutojihususha na matumizi hayo na kuepuka ngono zembe.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Serikali Prof. Mohamad Bakari Kambi amesema kuwa virusi vikubwa vya
ugonjwa wa ini ni A,B na C ambapo vimelea A huletwa na mtu asiye na
maambukizi kula chakula kisicho salama na kunnywa maji yasiyo salama.
Aidha Prof. Kambi amesema kuwa
virusi B na C vya ugonjwa wa homa ya ini husababishwa pale mtu asiye
na maambukizi kugusa majimaji au damu kutoka kwa mgonjwa mwenye ugonjwa
wa homa ya ini.
Maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya
Ini huadhimishwa Julai 28 kila mwaka Duniani na mwaka huu imebeba kauli
mbiu isemayo “TOKOMEZA HOMA YA INI” ambapo hapa nchini imeadhimishwa
jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment