Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akiwa na wataalam wa ujenzi wa daraja la
Kologombe linalounganisha Kijiji cha Gwata na Dololo wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za mji wa Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Tamisemi Selemani Jafo akiwa na walimu wa sekondari Gwata alipotembelea
kukagua ujenzi wa madaraja wilayani Kisarawe.
………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tamisemi Selemani Jafo amewataka wakandarasi wa ujenzi wa
miundombinu ya barabara na majengo katika halmashauri zote nchini
kuzingatia mikataba ya ujenzi, huku akiwaonya tabia ya kuchelewesha
kukamilisha miradi kwa wakati.
Jafo aliyasema hayo katika ziara ya kikazi ya kutembelea miradi ya barabara na madaraja wilayani Kisarawe.
Amesema Ofisi ya Rais, Tamisemi haitofumbia macho wakandarasi ambao wameshinda tenda za ujenzi na kuonesha uwezo mdogo.
“Pia hatutafumbia macho
ucheleweshaji wa miradi bila sababu yeyote ya msingi kinyume na
matarajio yaliyoainishwa ndani ya mkataba,”amesema Jafo
Naibu Waziri Jafo katika ziara
zake hivi karibuni ikiwemo ujenzi wa daraja la Twangoma lililopo wilaya
ya Temeke mkoani Dar es salaam amekuwa akisisitiza wakandarasi
kuzingatia ubora wa madaraja yanayojengwa nchini ili yaweze kudumu kwa
muda mrefu.
Jafo amemaliza ziara yake leo
wilayani Kisarawe na anatarajia kuendelea na ziara yake ya kikazi mkoani
Morogoro, Songwe, Njombe, Singida, Tabora, Kagera, Mwanza na Mara.
No comments:
Post a Comment