Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiwa na mchanga mkononi
akiwasikiliza maafisa wataalam katikati Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya
Makamu wa Rais ambaye pia ni katibu wake Bw. Daniel Sagata, na kulia ni
Afisa kutoka DAWASA Bw. Abel Chibelenge akieleza kuhusu uharibifu wa
mazingira unaofanywa na wananchi kati kati ya mto Mpigi katika eneo la
Mpaka wa Bagamoyo na Dar es Salaam, ambapo uharibifu huo Umeharibu eneo
ambapo limepita Bomba kubwa la maji safi (halipo pichani) linalo
safirisha maji kutoka Mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini na
kuhudunia seheu ya mkoa mkoa wa Pwani na Jiji la Dar es Salaam, Bomba
ambalo lipo hatarini kuharibika.
Afisa Mtaalam kutoka DAWASA Bw.
Abel Chibelenje (kulia) akimuonyesha Naibu Waziri Mpina Sehemu ya mto
Mpigi ( haipo Pichani, iliyoharibiwa vibaya kutokana na shughuli za
uchimbaji wa mchanga. (Picha na Evelyn Mkokoi)
………………………………………………………………………..
NA; EVELYN MKOKOI
Katika hali isiyoya kawaida,
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga
Mpina, amefanya ziara ya Oparesheni maalum kwa kushirikiana na jeshi la
Police kitengo cha FFU ili kuweza kubaini uharibifu wa mazingira
unaofanywa kwa uchimbani na uchotaji wa mchanga katika vyanzo vya maji
na maeneo mengine.
Akiwa katikati ya Mto Mpigi
uliopo katika mpaka wa Dar es salaam na Bagamoyo usiku wa kuamkia leo,
naibu Waziri Mpina alisema kuwa watu wanaochimba na kuchota mchanga
kiholelea watachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini
kwa mujibu wa sheria, kutaifishwa kwa magari yao na hata kufikishwa
mahakamani.
“kama mnavyoona hapa na kama
tulivyosikia kutoka kwa mtu wa DAWASA haya mabomba ya maji yanayopita
katika mito yanaharibika kutokana na shughuli hizi na serikali inaweza
kuingia gharama kubwa sana kurekebisha mabomba haya kama bomba hili
Mtaalam amesema hapa itagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 80
kutengeneza bomba hili.” Alisema Mpina.
Aidha Mpina alisema ukiachilia
mbali uharibifu wa Miundo Mbinu hiyo ya Maji pamoja na Mazingira
wananchi wnaweza pia kukosa maji kwa takribani muda wa wiki mbili.
“Mabomba haya yalikuwa chini ya
mchanga lakini kwa sasa hivi yananing’inia kutokana na uchimbaji wa
mchanga na mto unazidi kupanuka na maji yanakwenda kwenye makazi ya watu
na kusababisha mafuriko, na madhara kwa miundombinu mingine kama vile
ya umeme na barabara ambapo serikali imeijenga kwa gharama kubwa”.
Alisisitiza Mpina
Alongeza kwa kusema kuwa hakuna
mtu yoyote atakaye ruhusiwa kuchimba mchanga katika maeneo yasiyo
ruhusiwa na wanachi wajihepushe na uharibifu wa mazingira Mpina
alisisitiza kuwa serikali haizuii wananchi kuchimba mchanga bali
inakataza wanachi kuchimba mchanga kiholela na kuharibu mazingira.
Naibu Waziri Mpina alisema kuwa
uungwaji mkono wa sehemu nyingine ya serikali kama vile Halmashauri na
vyombo vingine vya ulizi na usalama ni mkubwa na ndo maana katika
opareshi hiyo hawakuweza kukuta shughuli zozote zikiendelea katika muda
huo,na wahalifu wameanza kuona kuwa serikali haina mzaha na ndiyo maana
team ya oparesheni hiyo imekuwepo katika eneo la tukio kwa muda huo wa
usiku.
“Oparesheni hii ni agizo na zoezi
hili litaenda Nchi nzima, na tumeanzia Dar es Salaam , Halmashauri zote
zinatakiwa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kufanyika kwa shughuli
hii.” Aliongeza Mpina.
Aliwaasa viongozi wasingojee Waziri NEMC au wa Viongozi wajuu kuwatembelea na kufanya zoezi hili.
Kwa upande wake Afisa kutoka
DAWASA Bwana Abel Chibelene wao kama wamiliki wamiundombinu hiyo ya maji
kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wamefanya jitihada za kutosha kwa
kushirikiana na vyombo vya ulinzai na usalama, na kufikia hatua ya
kuweka walinzia katika miundombinu hiyo lakini bado wananchi wamekuwa
wakiendelea na shugulizi hizo ambazo si salama kwa mazingira na
miundombinu hiyo muhimu ya maji.
Opareshi hiyo ya kamata kamata ya
wachimba mchanga, imeanzishwa na Naibu Waziri Mpina na kuwa ni agizo
kwa Halmashauri zote na miji nchini kutekeleza zoezi hilo
No comments:
Post a Comment