Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale Hamimu Gwiyama akifungua Mafunuzo ya siku Moja ya maafisa Ugani wilayani Nyang’wale mkoani Geita.
Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale Hamimu Gwiyama akiwa katika picha ya pamoja na maafisa Ugani walioshiriki katika mafunzo hayo.
………………………………………………………………………
Wito Umetolewa kwa Maafisa Ugani
waliopo katika Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita kutumia nafasi zao
vizuri katika kwa wakulima ili kuwafanya kulima kilimo cha kisasa
ambacho kina tija katika Jamii kwa ujumla.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa
wilaya ya Nyang’wale Hamimu Gwiyama wakati akifungua mafunzo kwa maafisa
Ugani 27 kutoka wilaya hiyo yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi
na teknolojia COSTECH kupitia Jukwaa la bioteknolojia la Kilimo(OFAB)
yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao nafasi yao katika kilimo ili
kutoa mbinu kwa wakulima kuwa na kilimo cha kisasa hasa katika mazao ya
mizizi.
Mh Hamimu alisema kwamba kuna
fursa nyingi katika Mkoa huo hasa zinazo husu kilimo kama wagani hao
wataweza kufanyia kazi ipasavyo mafunzo hayo watakayo pewa na wataalamu
basi wakulima wataanza kuneemeka.
“Zipo fursa nyingi katika wilaya
hiyo ambapo upo uwezekano wa kulima mazo ya Pamba,Dengu,Mahindi kama
mafunzo hayo mtafanyia kazi vizuri naamini njaa katika wilaya yangu ni
historia”Alisema Hamimu
Kwa upande wake Mratibu wa OFAB
Tanzania Philbert Nyinondi alisema wapo katika kutekeleza sera ya nchi
ya uchumi wa viwanda hivyo wameona ni vyema kutoa elimu namna ya kupata
kilimo cha kisasa na chenye tija ambacho kitainua pato la Taifa.
“Kikubwa kilichotuleta ni kuweka
makundi haya makubwa mawili kati ya wagani na watafiti ili kwa pamoja
waweze kujua namna ya kutataua changamoto ya kilimo ili kwenda katika
uchumi wa viwanda” Alisema Nyinondi
Hata hivyo baadhi wa wagani
katika wilaya hiyo wamesifu mafunzo hayo na kusema kwamba fursa za
kilimo zilizopo katika wilaya hiyo zitaenda vizuri kama bajeti
wakitengewa na kuweza kuwa na mashamba darasa kwa wakulima ambapo
itakuwa rahisi kwao kutoa elimu vizuri kwa wakulima
No comments:
Post a Comment