Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu
kinachomuelezea Jane Goodall na miaka 50 alioishi Gombe kutoka kwa
Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe
katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane Goodall. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na akiwa
kwenye kikao na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa
maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk. Jane
Goodall.Dk. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na
Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia
kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na
Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo Injinia Ngosi Mwihava. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana
na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na
mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dk.
Jane Goodall.
Dk. Goodall pamoja
na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu
jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na Dk. Jane
Goodall, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katika Ujumbe wake Dk. Goodall
aliambata na Mama Getrude Mongela na Hadija Simba ambao ni wajumbe wa
Bodi ya Taasisi ya Roots and Shoots pamoja na watendaji wengine wa
Taasisi hiyo.
Katika mazungumzo yao Dk. Goodall
pamoja na mambo mengine amezungumzia uharibifu wa shoroba za wanyama
pamoja na makazi yao katika hifadhi ya Gombe iliyopo mkoani Kigoma
ambayo ni maarifu kwa uhifadhi wa Sokwe. Alisema kwa sasa hifadhi hiyo
imezungukwa na maakazi ya binadamu hali iliyosababisha kupungua kwa
kiasi kikubwa kwa idadi ya wanyama hao.
Aidha Dk. Goodall alimuelezea
Makamu wa Rais jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake
katika kupambana na uharibifu wa mazingira katika hifadhi ya Gombe
ikiwemo kuhimiza uwepo wa mipango bora ya matumizi ya ardhi.
“inawezekana tatizo kubwa
linalosababisha uharibu wa mazingira ni umasikini na uelewa mdogo wa
wananchi” alieleza Dk.Goodall. Hata hivyo alisema zipo jitihada
mbalimbali zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kutoa elimu kwa umma.
Kwa sasa wananchi kutoka katika vijiji zaidi 52 mkoani wa Kigoma
wanapatiwa elimu kuhusu utunzaji wa mazingira. Vilevile, jumla ya
shilingi Milioni 400 zimekopeshwa kwa wananchi wa vijiji 32 ili
kujiwezesha kiuchumi na kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira
hususan yenye leno la kulinda shoroba na makazi ya Sokwe. Hali hii
imeanza kuleta mafanikio.
Dk. Goodall ametaja changamoto
kubwa katika uhifadhi wa mazingira ya Gombe kuwa ni kuwepo kwa wakimbizi
kutoka Burundi ambao kwa kiasi kikubwa hushiriki katika shughuli
ambazo husababisha uharibu wa mazingira kama vile kilimo na ufugaji usio
endelevu.
Kwa upande wake Makamu wa Rais
alisema serikali inafanya kazi kubwa katika kuhakikisha mazingira ya
hifadhi za Taifa pamoja na ikolojia yake yanatunzwa. Makamu wa Rais
amemhakikishia Dk. Goodall kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua
madhubuti ili kuhakiksha wananchi wanafanya shughuli za kujiletea
maendeleo bila kuharibu mazingira. “Ni muhimu kuishirikisha jamii
inayoishi pembezoni mwa hifadhi zetu katika suala la uhifadhi wa
mazingira lakini pia kuwa na mipango bora ya matumizi ya ardhi”, alisema
Makamu wa Rais. Kuhusu suala la wakimbizi kuharibu mazingira, Makamu wa
Rais aliahidi kutoa maelekezo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ili
kuona namna bora ya kulipatia ufumbuzi suala hilo.
Mwisho, Makamu wa Rais
alimpongeza Dk. Goodall kwa kupewa tuzo ya heshima na Mamlaka ya Hifadhi
za Taifa (TANAPA) kama ishara ya kutambua mchango wake katika masuala
ya uhifadhi wa Sokwe na mazingira kwa ujumla
No comments:
Post a Comment