Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi wa India
Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kushoto
ya Balozi Seif ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Zanzibar
Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar
{ZAWA} Dr. Mustafa Garu.
Balozi
Seif akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana
Sandeep Arya baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyomshirikisha Waziri
wa Elimu Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Maji Zanzibar Dr. Mustafa Garu.
Balozi
Seif wa Pili kutoka Kulia akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya aliyeko upende wa Kulia yake.
Wa
kwanza kutoka Kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma, wa kwanza kutoka Kushoto ni Balozi Mdogo
wa India aliyepo Zanzibar Bwana Setandar Kumar na Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Maji Zanzibar Dr. Mustafa Garu.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na Othman Khamis OMPR.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana kwa
mazungumzo na Balozi wa India Nchini Tanzania Bwana Sandeep Arya Ofisini
kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika
mazungumzo yao yaliyohudhuriwa pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali Zanzibar Mh. Riziki Pembe Juma na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji
Zanzibar {ZAWA} Dr. Mustafa Garu Balozi wa India Bwana Sandeep
alisisitiza umuhimu wa kuanzishwa miradi mipya itakayostawisha Jamii kwa
lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande hizo mbili.
Balozi
Sandeep alisema India hivi sasa imejipanga kuona miradi iliyoahidi
kuitekeleza kwa Tanzania ya huduma za Maji safi na Salama upande wa
Zanzibar pamoja na vifaa kwa ajili ya Vituo vya kazi za amali
inakamilika kwa wakati.
Alisema
uimarishaji wa Vituo vya Amali utatoa nafasi kubwa kwa Vijana kupata
mafunzo ya vitendo yatakayowajengea uwezo mpana wa kujipatia ajira
badala ya kusubiri kutoka Serikali Kuu.
Kwa
upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliishukuru Serikali ya India kwa uamuzi wake wa kuendelea kuiunga mkono
Zanzibar na Tanzani kwa ujumla katika kusaidia miradi ya Maendeleo.
Balozi
Seif alisema Miradi ya Maji safi na Salama Visiwani Zanzibar pamoja na
Msaada wa Vifaa kwa ajili ya Vituo vya Amali Nchini ni masuala ya
msingi kwa wakati huu katika kuimarisha ustawi wa Wananchi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimueleza Balozi huyo wa India Nchini
Tanzani kwamba Zanzibar bado inaendelea kuhitaji vifaa vya Kilimo kama
Matrekta kwa lengo la kusaidia nguvu za Wakulima katika sekta ya kilimo.



No comments:
Post a Comment