Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Kijana
Khamis Mgaya Juma aliyelazwa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmmoja baada ya
kushambuliwa na Vijana Mtoni Kidatu Jumanne ya Tarehe 11 Julai 2017.Wa
kwanza kutoka kulia anayemsaidia Mgonjwa Khamis ni Baba Mzazi Mzee
Mgaya Juma na kulia ya Balozi Seif ni Muuguzi wa Zamu ya Wagonjwa wa
Wodi ya Mifupa Biubwa Hassan Juma.
Majeruhi
Khamis Mgaya Juma aliyelala kitandani akimuelezea Balozi Seif Mkasa
uliomkubwa wakati aliposhambuliwa kwa mapanga na Vijana wasiopungua Saba
Eneo la Mtoni Kidatu na kumjeruhi sehemu za Kichwa, Mikono na Miguu.
Balozi
Seif akiwaagiza wauguzi kuzingatia maadili yao ili kupunguza malalamiko
yanayotolewa na wagonjwa wakati akimfariji Kijana Khamis Mgaya
aliyejruhiwa kwa mapanga Jumanne iliyopita.(Picha na OMPR.
Na. Othman Khamis OMPR.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameliagiza Jeshi la
Polisi Nchini kuwasaka na kuwatia mikononi mara moja Vijana
Waliohusika na kitendo cha kinyama cha kumshambulia kwa Mapanga Utingo
wa Dala dala ya bara bara ya Mtoni Kidatu - Darajani Kijana Khamis
Mgaya Juma mnamo Tarehe 11 Julai 2017.
Alisema
kitendo hicho ambacho hakikubaliki kibinaadamu hata kisheria
kinastahiki kulaaniwa na Jamii nzima na Serikali Kuu kupitia vyombo vya
Ulinzi haitakubali kuona tabia kama hiyo inaendelea kushuhudiwa Mitaani.
Balozi
Seif Ali Iddi alitoa agizo hilo wakati alipofika Hospitali Kuu ya Mnazi
Mmoja kumkagua na kumfariji Kijana Khamis Mgaya Juma mwenye umri wa
Miaka 24 aliyepata mtihani huo akiwa kazini mwake Hapo Mtoni Kidatu
Wilaya ya Magharibi “A”.
Khamis
Mgaya licha ya kupata majeraha makubwa sehemu za Kichwa, Miguu pamoja
na mikono yote miwili baada ya kushambuliwa kwa silaha za jadi za
Mapanga na Vijana zaidi ya Saba hivi sasa anaendelea kupata nafuu licha
ya kubakiwa na maumivu katika mwili wake.
Balozi
Seif alisema polisi licha ya doria wanazoendelea kuzifanya sehemu mbali
mbali Nchini lakini bado kuna haja ya kuafuatilia nyendo za watu
wanaoripotiwa kwao kuhusika na vitendo viovu ikiwemo ujambazi.
Alisema
hatua hiyo kwa kiasi kikubwa inaweza ikatoa fursa kwa wananchi kuwa na
amani pamoja na utulivu wa kuendelea na harakati zao za Kimaisha bila ya
wasi wasi wote.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alimtakia matibabu mema Kijana Khamis Mgaya
Juma na kumuomba aendelee kuwa na subira wakati huu wa maumivu wakati
Serikali kupitia vyombo vya Ulinzi vitahakikisha wale wote waliohusika
na tatizo lililomkubwa wanaonja mkono wa sheria.
Balozi
Seif halkadhalika waliwakumbusha Madaktari na Wauguzi kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia maadili bila ya kujali wanao muhudumikia ana
wadhifa au cheo gani.
Alisema
baadhi ya Madaktari hasa wauguzi wamekuwa wakiripotiwa kuhusika na
vitendo vya kunyanyasa wagonjwa mambo ambayo yako nje ya maadili yao ya
kazi.
Balozi
Seif alisema Serikali imetoa msukumo wa kuwapatia Wananchi matibabu
bure lakini bado wapo baadhi ya watu dhana hiyo wamekuwa wakiiwekea
vikwazo visivyo na msingi kwa kuwasumbuwa Wananchi hao.
Mapema
Majeruhi Khamis Mgaya Juma alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar kwamba alipatwa na kasa huo Jumanne ya Tarehe 11 Julai baada
ya Mmoja wa abiria aliowachukuwa kwenye Gari yake kukataa kulipa Nauli.
Kijana
Khamis alisema licha ya kumsamehe Kijana huyo baada ya kubishana muda
wote wa safari lakini Abiria huyo aliamua kutafuta Vijana wenzake na
kupanga njama ya kutaka kumfanyia hujuma wakati akiendelea na harakati
zake za kazi.
Alisema
Vijana hao walilazimika kukodi gari kumfuatilia Utingo huyo na hatimae
kufanikiwa kumavia wakati wakishusha Abiria katika maeneo ya Mtoni
kidatu wakitokea Mjini Darajani.
Khamis
alielezea masikitiko yake pale alipoomba msaada kwa wasamaria waliopo
katika na eneo hilo la tukio wakati akiendelea kushambuliwa kwa mapanga
lakini wazee waliokuwa karibu ya tukio hilo walihamasisha Vijana hao
kuendelea kumpiga.



No comments:
Post a Comment