Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL Pesa uliofanyika
Makamu Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba. (Picha na Ofisi ya
Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa huduma ya TTCL Pesa uliofanyika
Makamu Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar es Salaam. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa TTCL Pesa uliofanyika Makamo Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar Es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba (kulia) akimuonesha namna
ya kutumia huduma ya TTCL Pesa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi
wa TTCL Pesa uliofanyika Makamo Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini
Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Afisa
Mtendaji Mkuu wa TTCL Ndugu Wazir W. Kindamba (katikati) pamoja na
Mwenyekiti ya Bodi ya TTCL Mhe. Omari Nundu wakimuonesha kwa vitendo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan jinsi pesa inavyotumwa na kupokelewa kupitia huduma ya TTCL Pesa
mara baada ya kukamilika kwa uzinduzi wa TTCL Pesa uliofanyika Makamo
Makuu ya TTCL barabara ya Samora jijini Dar Es Salaam. (Picha na Ofisi
ya Makamu wa Rais)
………………………………………………………………..
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amezindua huduma mpya
ya fedha mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA ya Kampuni ya Simu Tanzania
TTCL. Uzinduzi huo umefanyika katika Makao Makuu ya TTCL barabara ya
Samora jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Omari Nundu
ambaye ni Mwenyeketi wa Bodi ya TTCL, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujezi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete, Afisa Mtendaji Mkuu
wa TTCL Bwana Waziri Kindamba, Wajumbe wa Bodi na wafanyakazi wa TTCL.
Akizungumza katika hafla hiyo
Makamu wa Rais alisema uzinduzi wa huduma ya TTCL PESA ni mwendelezo wa
jitihada za Kampuni hiyo kurejea katika nafasi yake ya awali ya kuwa
suluhisho la kweli la utoaji huduma za Mawasiliano hapa nchini.
“Kuzinduliwa kwa huduma hii ni
uthibitisho mwingine kwamba, TTCL inatekeleza kikamilifu maagizo ya
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe
Magufuli ambaye ameelekeza kuwa, Mashirika yote ya Umma yajiendeshe kwa
faida, yatoe gawio Serikalini, yawahudumie wananchi kwa kiwango cha
juu kabisa cha ubora na kwa gharama nafuu” alisema Makamu wa Rais.
Aidha, Makamu wa Rais alisisitiza
kwamba TTCL PESA itawezesha wananchi kutuma na kutoa pesa kwa viwango
vya chini kabisa kupita mitandao yote, pia itawezesha wananchi kulipia
Bill za Umeme (LUKU), Maji, Ving’amuzi na kuwezesha wateja kununua muda
wa maongezi na vifurushi vya data vya TTCL. Aliwataka TTCL kuendelea
kuwa wabunifu zaidi ili waweze kuongeza huduma nyingine kadiri mahitaji
na siku zinavyokwenda.
Akijibu kuhusu changamoto
zilizotajwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Makamu wa Rais alisema
Serikali inazijua na itaendelea kuzipatia majawabu. Hatahivyo aliwataka
watumie vyema rasilimali walizopewa ikiwamo Mkongo wa Taifa na Kituo cha
Kuhifadhia Kumbukumbu za kimtandao kupata pesa za kujiendeshea.
Makamu wa Rais pia aliipongeza
menejimenti ya TTCL kwa wazo lao la kufikiria kuanzisha kiwanda cha simu
hapa nchini. Alisema “msisitizo wa serikali yetu kwa sasa ni ujenzi wa
uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025 kupitia uwekezaji katika viwanda
hivyo wazo lenu la ujenzi wa kiwanda cha simu limekuja wakati muafaka”.
Mwisho, Makamu wa Rais alisema
TTCL PESA itatoa fursa kubwa ya ajira kwa wananchi kuwa mawakala na
itarahisisha shughuli za kiuchumi hasa biashara na hivyo aliwasihi
wananchi kuonesha uzalendo wao kwa kutumia huduma za TTCL.
Baada ya uzinduzi huo Makamu wa
Rais alishiriki katika Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Linah George
Mwakyembe ambaye ni mke wa Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo iliyofanyika katika kanisa la KKKT
Kunduchi Beach, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment