Mmiliki wa Kiwanda cha Chobo
Investment, Bw. John Chobo (mbele) akiwaongoza viongozi wa Benki ya
Kilimo kutembelea kiwanda hicho. Aliofutana nao ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara
na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kushoto).
Ugeni kutoka TADB ukijionea nyama iliyohifadhiwa kwenye jokofu (chiller) kusubiri kuchakatwa kabla kupelekwa sokoni.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha
Chobo, Bw. Charles Hotar akionesha mashine ya kuchakatia nyama kwa ajili
ya kutengenezea soseji kwa wageni kutoka Benki ya Kilimo (hawapo
pichani).
Mtaalamu kutoka Idara ya Soseji wa wa Kiwanda cha Chobo, Bw. Stanley Kirio akiendelea na zoezi la kuandaa soseji.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha
Chobo, Bw. Charles Hotar (kushoto) akionesha soseji zilizokuwa katika
hatua za ufungaji. Wanaomuangalia ni wageni kutoka Benki ya Kilimo.
Mmiliki wa Kiwanda cha Chobo
Investment, Bw. John Chobo (kulia) akiwaonesha vifungashio vya soseji
zilizotayari kupelekwa sokoni. Wanaomtazama ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) na Mkurugenzi wa
Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akionja soseji za Kiwanda cha Chobo.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Chobo wakichapa kazi.
……………………………………………………
Na mwandishi wetu, Mwanza
Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) imesema imeridhishwa na uwekezaji wa Kiwanda cha Nyama
cha Chobo kilichombo Misungwi jijini Mwanza kwa kuwa kinawahakikishia
wakulima wadogo masoko ya mifugo yao.
Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati alipofanya ziara
ya kujionea maendeleo ya uwekezaji wa miundombinu ya Kiwanda hicho.
Bw. Assenga amesema kuwa Kiwanda
cha Chobo ambayo inamilikiwa na kijana mzalendo, John Chobo ina uwezo
mkubwa wa kusadia wakulima wadogo kwa kununua mifugo yako hivyo
kuwapatia fursa za masoko wakulima hao.
“Miundombinu ya Kiwanda inaweza
kuchinja zaidi ya ng’ombe 600 kwa siku, hili ni soko kubwa sana kwa
wakulima wadogo wa mikoa ya Kanda ya Ziwa hali itakayounga mkono juhudi
za serikali hasa TADB katika kuboresha minyororo ya thamani kwenye sekta
ya mifugo,” alisema.
Bw. Assenga amesema Serikali
iliamua kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili
kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha
upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi
katika kilimo nchini.
Bw. Assenga ameongeza kuwa sekta
ya mifugo ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa
ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika
uongezaji wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa nchini.
Ameongeza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa.
“Benki inatoa mikopo na kusaidia
uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo
ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja
na usindikaji wa nyama na maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani nyama na
maziwa,” alisema Bw. Assenga.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo,
Mmiliki wa Kiwanda hicho, Bw. John Chobo alisema kuwa kwa sasa kiwanda
chake hakijafikia uwezo wa kutumika kwa asilimia 100 kutokana na
changamoto za kimtaji zinazomkabili na alitumia fursa hiyo kuiomba Benki
ya Kilimo kumuwezesha ili aweze kutoa ajira zaidi kwa Watanzania.
Kwa mujibu wa Bw. Chobo kwa sasa
kiwanda chake kina wafanyakazi 85 na kikifikia uwezo wa kuzalisha kwa
asilimia 100 kitaweza kuajiri zaidi ya wafanyakazi 300 watakaofanya kazi
kiwandani na 300 watakaokuwa wakisimamia shamba.
“Tunaiomba TADB kutatulia
changamoto za ukosefu wa mitaji ya uhakika kwa kuwa kwa kiasi kikubwa na
mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa
biashara za bidhaa na ambayo riba yake ni kubwa sana.,” alisema.
No comments:
Post a Comment