Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akisalimiana na Mbunge wa viti Maalumu Chadema, Mheshimiwa Upendo
Peneza, katika mkutano wa hadhara uliyofanyika Ruangwa Mjini, akiwa
kwenye ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, Julai 12, 2017. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
………………………………………………………………..
MBUNGE viti Maalumu Chadema,
Mheshimiwa Upendo Peneza amewaomba wananchi waliombee Taifa liendelee
kuwa na amani pamoja na kuwaombea viongozi wa kisiasa wawe na uvumilivu
ili wazidi kusonga mbele kimaendeleo.
Aliyasema hayo jana (Jumatano,
Julai 12, 2017), katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa shule
ya msingi Likangara wilayani Ruangwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa mkoani Lindi.
“Wananchi wa Ruangwa nawatakia
maisha mema ili mzidi kusonga mbele, tuombee amani ya nchi yetu na
mtuombee viongozi tuwe na uvumilivu wa kisiasa.”
Mbali na Mheshimiwa Upendo, pia
mkutano huo uliudhuriwa na wabunge wengine ambao ni Mheshimiwa Hassan
Masala (Nachingwea), Mheshimiwa Zubery Kuchauka (Liwale), Mheshimiwa
Hassan Kaunje (Lindi Mjini) na Mheshimiwa Hamida Abdalaah (Viti
Maalumu).
Kwa pamoja wabunge hao walisema
lengo la kushiriki kwenye ziara hiyo ni kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano katika kuwaletea wananchi
maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Lindi, Bw. Godfrey Zambi aliwataka wananchi wa mkoa huo kuhakikisha
wanaendelea kudumisha na kuilinda amani iliyoko kwa sababu ndiyo
inayowawezesha kufanya shughuli zao za kimaendeleo.
Alisema licha ya kuwepo kwa
matukio machache ya uhalifu yanayojitokeza katika baadhi ya maeneo
vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushirikiana na mikoa jirani
limejizatiti kukabiliana na wahalifu wa aina yoyote kwa mtu mmoja mmoja
au vikundi
No comments:
Post a Comment