• Breaking News

    ..

    ..

    Thursday, 13 July 2017

    WAZIRI MKUU MAJALIWA ASEMA TATIZO LA UMEME LINDI NA MTWARA KUWA HISTORIA, MRADI WA UMEME WA MAHUMBIKA NI MKOMBOZI

     NA K-VIS BLOG, Lindi
    WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea kituo cha kupoza na
    kusafirisha umeme kilichoko kijiji cha Mahumbika kilichoko Wilaya ya Lindi na
    kusema tatizo la kukatika umeme mikoa ya Lindi na Mtwara kumalizika kabisa
    ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika.
    Waziri Mkuu ambaye alitembelea mradi huo jioni ya Alhamisi Julai
    13, 2017, alisema mradi huo utakapokamilika, uwezo wa kusafirisha umeme
    utafikia Msongo wa Kilovoti 132, kutoka Msongo wa kilovoti 32 za sasa.
    Waziri Mmju alisema azma ya Serikali kupitia Shirika lake la umeme
    TANESCO ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa umeme kote nchini ili Watanzania
    wapate umeme mwingi na wa uhakika utakaosambazwa hadi vijijini na kwa gharama
    nafuu.
    “Mikoa wa Lindina Mtwara ilikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa
    umeme mara kwa mara mradi huu ni mkombozi kwa wana Lindi na Mtwara,
    tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza kwa sababu sasa nishati ya umeme ni ya
    uhakika.” Alisema Mhe. Majaliwa.
    Alisema mradi huo umegharimu kiasi cha Sh. bilioni 16 fedha za
    walipa kodi wa Tanzania.
    Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James
    Mdoe amesema mradi huu utawezesha kuimarika kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika
    na hivyo kuwahakikishia Watanzania kuwa safari ya kuelekea ujenzi wa uchumi wa
    viwanda ni ya uhakika.


    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu
    Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe, wakati alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika
    kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi,
    akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri
    Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku
    nne (katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye. 13, 2017. (Picha na
    Ofisi ya Waziri Mkuu)
     Mhe. Waziri Mkuu, akikagua mradi huo wa Mahumbika.
     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha
    Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Jafary Msuya, wakati alipotembelea mradi huo unaojengwa katika kijiji cha
    Mahumbika wilayani Lindi
    , Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017. (Picha na Ofisi ya
    Waziri Mkuu)

    Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya mradi wa kuzalisha umeme unaojengwa katika kijiji cha
    Mahumbika wilayani Lindi kutoka kwa Mhandisi Ferdinand Mwinje, wakati akikagua mradi huo unaojengwa katika kijiji cha
    Mahumbika wilayani Lindi
    , Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne 13, 2017. (Picha na Ofisi ya
    Waziri Mkuu)

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI