Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Hashimu Mgandilwa azindua mpango Kabambe wa
uchangiaji uzoaji taka kwa kwenye wilaya hiyo, ambapo kila kaya
itatakiwa kutoa shilingi mia moja kwa siku sawa na 3000 kwa mwezi.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam DC Mgandilwa ameeleza kuwa mpango huo utasaidia
kupunguza suala la uchafu katika wilaya hiyo na gharama zake ni nafuu
tofauti na awali ambapo kaya moja kwa kata ya Kibada walilazimika kulipa
kiasi cha shilingi elfu 20000 mpaka 40000 jambo ambalo ni changamoto
kwa wakazi hao.
DC
Mgandilwa ameeleza kuwa mradi huo utasaidia changamoto iliyojitokeza ya
baadhi ya watu kutupa taka kwenye fukwe ya bahari, huku akiwaomba
wananchi katika kaya mbalimbali kutunza taka zinazozalishwa majumbani
mpaka magari ya mradi yatakapokuja kuzichukua zikiwa katika mazingira
mazuri, ambapo amesema kwa kufanya hivyo kutaifanya wilaya ya Kigamboni
kuepuka Magonjwa ya mlipuko.
DC
Mgandilwa ameisisitiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha mradi huo
unakuwa ni wa uhakika kwa kutosuasua na kuhakikisha kata zinazolewa kwa
wakati na hayo magari manne ya awali yasambazwe maeneo mbalimbali ili
huduma stahiki ziwafikie wananchi.
DC Mgandilwa ameongeza kuwa Halmashauri haina uwezo wa kutoa msisitizo kila wakati ili watu watunze Mazingira hivyo ni jukumu la wanakigamboni kutunza mazingira, ambapo amewaomba wananchi kulipa kiasi hicho cha 3000 kwa mwezi kiasi ambacho mwananchi wa kawaida anaweza kumudu, vile vile kwa wamiliki wa Hoteli na taasisi mbalimbali wamewekewa kiasi ambacho ni nafuu kwao.

Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Steven Katemba ameeleza kuwa
mradi huo utawanufaisha vijana zaidi ya 134 na utaanza kwa kata tano
ikiwemo Kigamboni, Mjimwema, Tungi, Kibada na Vijibweni.
Huku
akieleza kuwa mpango wa baadae ni kuwa na Dampo la Lingato ambapo
bilioni moja imetengwa na Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya ukarabati wa
dampo hivyo ndani ya miezi kadhaa ukarabati utakwisha na taka hazitakuwa
zinapelekwa Kata ya Tungi.
No comments:
Post a Comment