
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi ya kisasa ya kinamama na watoto inayojengwa Hospital ya Amana yenye thamani ya shilingi Billion 1.2 ambapo ujenzi wake umekamilika kwa 100%.
Wodi
hiyo ya kisasa itakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 150 ambapo ndani
yake kutakuwa na Vifaa vya kisasa vya kutolea huduma, Vyumba vya
Madaktari,vyoo vya kisasa,mabomba ya maji, taa za kisasa na sehemu ya
kutosha ya wagonjwa kukaa wakati wakisubiri kuhudumiwa.
Ujenzi
wa Wodi hiyo ni unafadhiliwa na Kampuni tanzu ya Mafuta na Saruji ya
Amsons Group ambayo imekubali kumuunga mkono Mheshimiwa Makonda kwa
kujenga wodi tatu wazazi na watoto kwenye Hospital za Amana, Temeke na
Mwananyamala ambapo zote zitakuwa na uwezo wa kuchukuwa vitanda 450.
“Ujenzi
huu na hatua iliyofikia inatoa matumaini mapya kwa kinamama, watoto na
wakazi wa Dar es salaam juu ya upatikanaji wa huduma bora na nzuri
kwenye Hospital zetu za Serikali,watu walishazoea huduma nzuri
zinapatikana nje ya Hospital za Serikali lakini kwa sasa hali
itabadilika, na nina uhakika ndani ya muda mfupi tutamuomba Rais
Dr.Magufuli aje atuzindulie hizi wodi kama ishara ya kumbukumbu ya kazi
aliyoianza alipotembelea Hospital ya Muhimbili na kukuta watu wamelala
chini na kutafuta majibu, sisi wasaidizi wake ametupa kazi ya kutatua
kero za wananchi, hivi ndivyo tunavyozitatua kwa vitendo” Alisema.
Aidha
Makonda amesema wodi hiyo itazidisha upatikanaji mzuri wa huduma bora
za Afya kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam huku akieleza kuwa lengo
lake ni kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa mkoa unaotoa huduma bora za
Afya.
“Kama mnakumbuka wakati tunakuja wodi
iliyokuwa ikitumik akinamama walikuwa wakilundikana chini na wengine
wanatumia kitanda kimoja zaidi ya watatu hadi wanne na wakati mwingine
walikuwa wakilazimika kurudi nyumbani kabla ya muda wa madaktari
kuruhusu kutokana na mazingira duni yaliyokuwa yakikabili wodi hiyo,
lakini wodi hii itamaliza kero hiyo” Aliongeza Makonda.
ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi
ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa wodi
Hata
hivyo Makonda amewataka wadau wa maendeleo wenye dhamira ya kuchangia
shughuli za Maendeleo kwenye Mkoa wa Dar es salaam kujitokeza kwa wingi
Ofisini kwake na Ofisi za Wilaya kuungana na Serikali kuujenga Mkoa huo
“Nawapongeza
watumishi na wafanyakazi wa Afya kwenye Hospital za Amana, Temeke na
Mwananyamala kwa kazi kubwa wanayoifanya kupunguza kero kwenye Sekta ya
Afya” Alisema Makonda.
No comments:
Post a Comment