• Breaking News

    ..

    ..

    Wednesday, 26 July 2017

    RC Makonda ametengua nafasi za maafisa elimu kata 12 jijini Dar es salaam

    Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ametengua nafasi za maafisa elimu kata 12 kutoka katika kata ,mbali mbali zilizopo jijini Dar es salaam.

    Rc Makonda amefanya maamuzi hayo alipo kua anedelea na mkutano wa wakuu wa shule za Msingi na sekondari, na maafisa elimu kata hii leo.

    Chanzo cha kuwasimamisha nafasi zao ni kutokana na kudai malipo ya posho zaidi na wao wanavyopewa hivi sasa ya kima cha shilingi laki mbili na nusu, fedha kwajili ya posho ikiwa ni nje ya mishahara yao 


    lakini wamelalamikia mbele ya mkuu wa mkoa kuwa Haziwatoshi katika kufanya shuhuli zao za kimaendeleo ya elimu kwa kata zao .

    jambo ambalo lilipelekea kutofautiana baina ya maafisa elimu kata hao ambao jumla ya idadi yao ni 28 lakini hao 12 kati yao walikataa wakitaka kuongezewa kwa posho hiyo.

    Hata hivyo Rc makonda amemwagiza Afisa elimu wa mkoa kuwavua vyeo vyao wote 12 na kuwapangia majukumu mengine na kumta afisa elimu kuwapa adhabu nyengie tofauti na hiyo kisha afanye utaratibu wa kujaza nafasi zao kwa haraka.

    No comments:

    Post a Comment

    HABARI

    HABARI

    MICHEZO

    LOGO

    LOGO

    MAOJIANO

    BURUDANI