Serikali kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeanzisha rejesta ya
wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu itakayowekwa katika kila
ngazi ya utoaji wa huduma za Afya hapa nchini.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameyasema hayo, leo Mjini
Dodoma, katika mkutano wa kupitia utekelezaji wa mkakati wa uboreshaji
wa kasi ya uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu nchini.
Ummy amesema Serikali inayo wajibu wa kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa kwa ufanisi uliokusudiwa, ili kufikia lengo hilo.
Kutokana nna dhamira hiyo njema
Wizara kwa mara ya kwanza imeanzisha rejesta mpya ya wanaohisiwa kuwa na
kifua kikuu itakayowekwa katika kila ngazi ya utoaji wa huduma za Afya
hapa nchini.
“Tayari rejesta hizi zimesambazwa na kuanza kutumika katika mikoa 16 iliyoanza kutekeleza zoezi hili,” amesema Ummy.
Waziri Ummy aliongeza kuwa mkakati
wa uboreshaji kasi ya uibuaji wagonjwa wa kifua kikuu ni mkakati
uliojaa mbinu za kiuendeshaji ili kuvipa uwezo vituo vya huduma za Afya
kufanya uchunguzi wa kina kwa kila mteja anayepata huduma vituoni na
kuwapata wote wenye kuugua kifua kikuu na kuwaanzishia matibabu.
Ummy amesema mkakati huo
unahusisha zana zinazotoa mwanga na kuangaza njia bora za kuchunguza
kifua kikuu na kubaini wote wenye kuugua katika jamii mijini na
vijijini.
Vile vile amesema, mkakati huo
umejaa mbinu za kiuendeshaji ili kuvipa uwezo vituo vya huduma ya Afya
kufanya uchunguzi wa kina kwa kila mteja anayepata huduma vituoni na
kuwapata wote wenye kuugua kifua kikuu pamoja na kuwaanzishia matibabu.
Pia utatoa fursa kwa kila kitengo
kujitathmini ili kuweka misingi timilifu ya uchunguzi wa kifua kikuu kwa
wateja wote wanaohudhuria matibabu katika eneo husika.
Aidha, amesema kuwa utekelezaji wa
mkakati huo ulianza mnamo Julai, 2016, ambapo ni mwaka mmoja sasa tokea
vituo vya mwanzo katika Mikoa ya Mbeya na Dodoma ianze kuweka msukumo
mpya. Kuanzia hapo, Mikoa 16, wilaya 48 na vituo 187 nchini kote
vimeweza kuanza utekelezaji.
Masuala ya ubora wa huduma za afya
yamepewa kipaumbele katika mkakati mpya uliotolewa na Shirika la Afya
Duniani wa kutokomeza kifua kikuu ifikapo mwaka 2035.
No comments:
Post a Comment