
Mkurungezi mtendaji Mkuu wa (GEL) Abdulmalick Mollel akimuelezea Huduma za Taasisi hiyo Dr.Charles Msonde ambaye ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa Mitihani( NECTA) wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na (TCU) Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

Mfanyakazi wa Taasisi ya Global Education Link Bw. Liberius John akiwa anatoa maelezo kwa wateja waliotembelea banda hilo ili kujionea huduma zinazotolewa na (GEL)

Baadhi ya wanafunzi na wananchi waliotembelea maonyesho hayo wakipata maelezo wakati walipotembelea banda la Global Education Link.

Wafanyakazi Mbalimbali wa Taasisi ya Global Education Link wakiwa kwenye banda hilo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wanaotembelea maonyesho ya Vyuo vikuu yanayofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam, Maonyesho hayo yameandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU)
…………………………………………………………………………………………….
Global Education Link (GEL) ambao ni mawakala wa Vyuo Vikuu vya Nje imesema kuwa kwa wanafunzi wanaotaka kufanyiwaudahili ili kujiunga na vyuo vikuu vya nje wanaweza kufika katika banda la na kupata maelezo hukusu vyuo hivyo katika maonesho ya TCU jijini Dar es salaam ,wanafunzi,wazazi na walezi mnakaribishwa ili kupewa miongozo ya udahili wa vyuo vikuu nje ya nchi,katika ngazi ya diploma mpaka shahada ya udhamili.
Akizungumza Mkurungezi wa Global Education Link(GEL),Abdulmalik Mollel amesema katika dhima ya serikali ya awamu ya tano ya viwanda inahitajika rasilimali watu wa kutosha ili kukidhi mahitaji hayo
Mollel amesema wanafunzi wanaohitaji kwenda kusoma nje ya nchi wajitokeze katika viwanja vya Mnazi Mmoja na kukutana na timu nzima ya Global Education Link kwa ushauri na utaratibu wa udahili wa papo kwa papo
No comments:
Post a Comment