KA
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg. Ally J. Ally amewataka wananchi kutoka pande zote za nchi ya Tanzania kulitembelea na kujionea vitu vya kipekee katika banda la Manispaa ya Ubungo katika wiki ya maonyesho ya wakulima nanenane yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kata ya Tungi Manispaa ya Morogoro kuanzia tarehe 01/08/2017 na kufikia kelele chake tarehe 08/08/2017.
Kauli hiyo aliitoa ofisini kwake Kibamba CCM alipokuwa akihojiwa juu ya maandalizi ya nanenane kwa Manispaa ya Ubungo.
Kaimu Mkurugenzi alisema Manispaa hiyo imefanya maandalizi ya kutosha na wananchi watarajie kuona vitu vya kipekee vilivyoandaliwa na wataalamu wa Manispaa hiyo.
"Ndugu wana Ubungo na watanzania kwa ujumla naomba mjitokeze kwa wingi kujionea yatakayojiri katika banda la UMC kwenye maadhimisho ya sikukuu ya wakulima (nanenane) yanayotarajiwa kuanza tarehe 01/08/2017 na kufikia kilele chake tarehe 08/08/2017 " alisema Kaimu Mkurugenzi na kuendelea,
" Manispaa ya Ubungo tumejiandaa vya kutosha juu ya maonyesho hayo, banda letu na vitu vyetu tulivyoandaa ni vya kisasa kwa hiyo ewe mwananchi usikubali kuhadithiwa karibu katika banda letu ujionee utofauti" alisema Kaimu Mkurugenzi.
Mwisho aliwataka wananchi kuhudhuria kwa wingi katika maonyesho hayo ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali kama kilimo mjini na kitalu nyumba (green housing) na mengine mengi.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA UHUSIANO UMC

No comments:
Post a Comment