Uchaguzi mkuu nchini Kenya utafanyika mnamo tarehe 8 mwezi Agosti.
"Enyi wasimamizi wa makundi ya WhatsApp ambao makundi yenu yanatumiwa kusambaza ujumbe wa chuki, hebu tuwe makini," amesema mwenyekiti wa tume hiyo Francis Kaparo, ambaye zamani alikuwa spika wa bunge la Kenya.
Amesema tume hiyo imeyatambua makundi zaidi ya 21 ya WhatsApp ambayo yanatumiwa kueneza chuki.
Bw Kaparo pia amewaonya wanasiasa ambao watatoa matamshi ya uchochezi, matusi, taarifa za uongo, yanayodhalilisha mtu au watu kingono au ya kukudunisha kikabila.
Bw Kaparo amesema "watakiona cha mtema kuni".
Aidha watumiaji wa simu za rununu pia wameonywa dhidi ya kusambaza ujumbe ambao unaweza kusababisha taharuki au vita vya kikabila.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Kenya Joseph Boinnet mapema leo Jumatatu, amesema kuwa kikosi chake "kitatumia nguvu zaidi" dhidi ya watakaosababisha vurugu.
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007/08, zaidi ya watu 1,133 waliuawa na zaidi ya watu nusu milioni wakaachwa bila makao baada ya ghasia kuzuka
No comments:
Post a Comment