Waziri Ummy amempongeza
Sophia Juma wa shule ya Sekondari Mazinde juu (Tanga) kwa
kushika nafasi ya kwanza, sanjari na Agatha Julius Ninga wa shule ya
Wasichana Tabora ambaye ameshika nafasi ya pili kitaifa.
Kadhalika, Waziri Ummy
amewapongeza wanafunzi wote wa kike kwa jitihada walizoonesha na
kuweza kufaulu mitihani yao kwa kiwango cha asilimia 97.21
ya waliofanya mtihani; ikilinganishwa na asilimia 95.34 ya
wavulana waliofaulu. Waziri ameeleza kufarijika na juhudi ya
wanafunzi wa kike, kufuatia ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu
kupanda kwa asilimia 94.07 katika madaraja haya ikilinganishwa na
wavulana waliofaulu kwa asilimia 93.49. Juhudi hizi sio za
kubezwa, na ni ishara thabiti kuwa mtoto wa kike akipewa nafasi hakika
anaweza.
Wizara inatambua
ushirikiano wa walimu, wazazi, na jamii ambao wamewezesha kufikiwa kwa
ubora wa ufaulu wa watoto wa kike. Juhudi zenu zimesaidia utekelezaji
wa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutoa fursa sawa kwa watoto
wa kike na wa kiume katika kupata haki ya elimu. Mhe.Ummy
amewasa watoto wa kike wa shuleni mbalimbali nchini kutafakari matokeo
ya mwaka huu ili kuwa chachu ya kujitambua na kujikinga na mimba
shuleni. Kama wanafunzi wa kike watajitambua watasoma kwa ari
kubwa kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Niwatake watoto wote wa
kike waelewe kuwa wamehitimu daraja moja, hata hivyo bado
wanalojukumu la kujiendeleza zaidi katika taaluma mbalimbali kama njia
ya kumwezesha mtoto wa kike na mwanamke kuchangia katika maendeleo ya
taifa kwa umahiri mkubwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
17/7/2017
No comments:
Post a Comment