Afisa elimu ya watu wazima mkoani
Pwani ,Hildelgade Makundi,akifungua mafunzo ya siku moja ya utambuzi wa
mradi wa elimu jumuishi kwa walimu 24 wa shule za msingi kutoka
halmashauri ya Kibaha mjini na Kibaha Vijijini .
Afisa
program uhamasishaji wa shirika la kimataifa linalotetea na kuhudumia
watu wenye ulemavu nchini (ADD)Isack Idama ,akizungumza katika mafunzo
ya siku moja ya utambuzi wa mradi wa elimu jumuishi kwa walimu 24 wa
shule za msingi kutoka halmashauri ya Kibaha mjini na Vijijini.
Walimu 24 kutoka halmashauri ya Mji wa Kibaha na Kibaha Vijijini Mkoani Pwani, walioshiriki katika mafunzo ya siku moja ya utambuzi wa mradi wa elimu jumuishi .
Picha na Mwamvua Mwinyi
……………………….
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAZAZI na walezi walio na watoto
wenye ulemavu ,wametakiwa kuwaandikisha watoto wao walio na sifa ya
kuanza elimu ya awali badala ya kuwaficha na kusababisha kukosa haki ya
kupata elimu.
Akizungumza katika mafunzo ya siku
moja ya utambuzi wa mradi wa elimu jumuishi kwa walimu 24 wa shule za
msingi kutoka wilaya ya Kibaha mjini na Vijijini,afisa program
uhamasishaji wa shirika la kimataifa linalotetea na kuhudumia watu wenye
ulemavu nchini (ADD)Isack Idama ,aliomba jamii ihamasike na kuibua
watoto hao.
Alieleza ,endapo tabia ya kuficha
watoto wenye ulemavu itaachwa itasaidia kupunguza idadi kubwa ya watoto
walio na ulemavu mbalimbali ambao hawajaandikishwa shule.
Kwa mujibu wa Idama,katika sensa
ya mwaka 2012 karibu asimilia 9.3 /10 ya watanzania milioni . 3.15
wanaishi na ulemavu mbalimbali.
Alisema kwamba,utambuzi wa watu
wenye ulemavu wa mwaka 2008 kati ya watoto 10 watoto wenye ulemavu
wanaopelekwa shule ni wanne pekee.
“Na kati ya watoto 10 wasio na
ulemavu 8-9 wanapelekwa shule hivyo kuna kila sababu ya kuibua idadi
kubwa ya watoto wenye ulemavu iliyopo majumbani ili idadi iwe sawa na
watoto wengine ”alisema Idama.
Idama alielezea kuwa,jamii itambue
umuhimu wa elimu kwa watoto wote bila kuwabagua wala kuwanyanyapaa ,na
kuwapeleka katika shule hasa za kawaida.
Aliiomba serikali kuwajengea
miundombinu rafiki ,kupeleka walimu wenye ujuzi maalum na vifaa lengwa
mashuleni kwa watoto wenye mahitaji hayo ili waweze kupata elimu bora.
Akizungumzia malengo ya mafunzo
hayo,alisema wamewapatia mafunzo walimu wa shule za msingi ambapo kila
kata wamechukua mwalimu mmoja ambao wataenda kufanya zoezi la utambuzi
wa watoto wenye ulemavu kuanzia miaka 3-6 kwa ajili ya kuanza elimu ya
awali.
Idama alibainisha,elimu jumuishi
itawezesha watoto hao kupata fursa ya kupata elimu sawa na kupatiwa
stadi na maarifa itakayowaandaa kwenda elimu msingi.
Awali akifungua warsha hiyo,kwa
niaba ya afisa elimu mkoani Pwani,afisa elimu ya watu wazima mkoani
hapo,Hildelgade Makundi alisema elimu jumuishi itawezesha kuondoa hali
ya kuwatenga watoto .
Hildelgade alieleza ,jitihada za
makusudi zifanyike kufichua watoto wanaofichwa ndani ya jamii ,Ushiriki
wa jamii uwepo ndipo mradi utakapofanikiwa na kuweza kuwatambua watoto
lengwa.
Kiongozi wa mradi wa elimu
jumuishi kutoka ADD,Victoria Lihiru alifafanua ,wanatekeleza miradi ya
elimu jumuishi kwa kufanyakazi na wizara ya elimu na TAMISEMI kuboresha
elimu .
Alisema wanafunzi wa shule za
awali 252 (chekechea)katika halmashauri nne ikiwa ni sanjali Mji wa
Kibaha,Mkuranga,Kibaha Vijijini na Kisarawe mkoani Pwani,zinatarajia
kunufaika na mradi wa kuongeza udahili wa watoto wenye ulemavu.
Victoria alisema kati ya shule hizo,shule 20 zitakuwa za mfano ambapo mradi utatekelezwa
kuanzia mwaka 2017-2021.
kuanzia mwaka 2017-2021.
Akitoa mada iliyohusu sheria namba
9 ya mwaka 2010 inayotoa msukumo wa upatikanaji wa haki kwa watu wenye
ulemavu ,mweka hazina wa shirikisho la vyama vya walemavu
Tanzania(SHIVYAWATA),Elias Masamaki alisema mtu mwenye ulemavu
anastahili kupata haki sawa ikiwemo afya na elimu .
anastahili kupata haki sawa ikiwemo afya na elimu .
Mmoja wa walimu walioshiriki
warsha hiyo,Winfrida Mkala kutoka shule ya msingi Mwendapole ,alisema
mradi wa ADD ikishirikiana na serikali utafanikiwa kama serikali
itaondoa changamoto za miundombinu ,walimu maalum na vifaa ikiwemo vya
kusikia na kusomea watoto walio na ulemavu.
Shirika la kimataifa la ADD ,lipo
nchini kwa takriban miaka 20 kwa ajili ya kutetea,fursa na usawa kwa
watu wenye ulemavu huku likifanya kazi na SHIVYAWATA
No comments:
Post a Comment